Sunday, November 5, 2017

UPIMAJI NA TATHIMINI , Tet05207. TTC director,. AY official


UPIMAJI KATIKA ELMU

Upimaji katika elimu ni kitu muhimu sana unapotaka kujua maendeleo yaliopatikana wakati wa kujifunza au kufundisha. Upimaji humuonyesha anaejifunza ni mahali gani amefanikiwa na ni mahali gani ana mapungufu. Vilevile anaefundisha anajua ni mahali gani amefanikiwa au niwapi hajafanikiwa.
MAANA YA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Katika elimu upimaji ni tendo la kutafuta ni kwa kiasi gani mwanafunzi amepata maarifa au stadi zilizofundishwa kufuatana na malengo ya ufundishaji wa mada za somo yaliyopo kwenye muhtasari. Upimaji katika elimu pia hujumuisha mwenendo na tabia ya mwanafunzi na uwezzo wake wa kufanya mambo mbalimbali.



Matokeo katika upimaji wa elimu hutumiwa na watu mbalimbali kwa mfano mwanafunzi,shule,wazazi,waajiri walimu na watafiti.

MWANAFUNZI
Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi
Huwa ni kigezo cha chake cha kutambua ameelewa kwa kiasi gani cha kitu au vitu/ mada alizofundishwa.
Huumpa changamoto ya kujifunza. Endapo amepata alama za juu hupenda kuziendelezana kama amepata alama za chini,hufanya bidii ya kujikwamua.
Huumfanya awe makini katika kujifuza maana anajua fika kuwa atapimwa. Hii humfanya asiwe mtoro au mzembe wakati wa masomo.

MWALIMU
Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi humuwezesha mwalimu.
Kutambuwa kiwango cha uelewa wa wanafunzi katika maada mbalimbali za somo.
Kutambua matatizo wanayopata wanafunzi wakati wa kujifunza na kuyatafutia ufumbzi.
Kutambua wanafunzi wenye matatizo ya kuelewa somo au sehemu ya somo ili aweze kuwapa mafunzo ya ziada.
Kugundua malengo ya somo ambayo wanafunzi hawakufanikiwa na kuchunguza sababu.
Kuangalia mapungufu na mafanikio ya mtaala na kutoa taarifa kwa wahusika.
Kurekebisha mbinu za kujifunzia na kubuni/ kufaragua vifaa vipya ili malengo mengi zaidi yafikiwe.
SHULE
Matokeo ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi huiwezesha shule
Kujua ufanisi wake katika elimu kwa kulinganisha na shule nyingine.
Kujua malengo ya mtaala yaliofikiwa.
Kupanga wanafunzi katika mikondo (si lazima wenye uwezo mmoja wakawa pamoja)
Kumshauri mwanafunzi kuendelea na ngazi ya masomo inayofuata au kurudia.
Kushauri viongozi wa elimu kuhusu mwanafunzi anaeonekana kuwa na uwezo au kipaji maalumu ili aweze kuendelezwa.
Kuwasiliana na mzazi kuhusu maendeleo ya mwanafunzi kwa kutumia ripoti.
Kushauri wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuhusu ubora au mapungufu ya mitaala ili hatua zinazofuata zichukuliwe.
MZAZI
Matokeo ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi humwezesha mzazi
Kufahamu maendeleo ya mtoto wake
Kuchunguza chanzo cha matatizo kama yapo na kushirikiana na shule kuyatafutia ufumbuzi
Kummotisha mtoto wake ili aongeze bidii.
MWAJIRI
Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi humwezezha mwajiri;
Kuchagua mfanyakazi kwa kuangalia uwezo wake kitaaluma na mwenendo tangu akiwa shuleni.
Kumpangia mfanyakazi aina ya kazi inayoendana na uwezo wake kitaaluma.

MADHUMUNI YA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Tunaweza kuorodhesha madhumuni ya upimaji katika elimu ambayo ni;
Kujua maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma, kitabia, na kistadi.
Kubaini matatizo ya mwanafunzi katika kujifunza.
Kuangalia kiwango cha kufanikawa cha malengo ya kila mada.
Kuamsha ari ya mwanafunzi kujifunza zaidi
Kuboresha ufundishaji.
Kuandaa vigezo vya kutumia wakati wa kuchagua wanafunzi kwa masomo ya juu au kozi mbalimbali.

NYANJA ZA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Katika elimu vipengele ya kuzingatia katika upimaji ni uwezo wa kitaaluma, kufanya vitendo,na kumudu matatizo au shinikizo mbalimbali katika maaisha.
Nyanja za upimaji ni maerneo ambayo ujuzi, mwelekeo na matendo tarajiwa kwa mwanafunzi kuwa nayo,kujenga au kupata baada ya mafunzo. Nyanja za utambuzi hujumuisha
Nyanja za utambuzi
Nyanja za mwekekeo
Nyanja za vitendo

NYANJA ZA UTAMBUZI
Nyanja hiii inahusika na ujuzi /uzoefu ambao mwanafunzi anatarajiwa kuwa nao baada ya kujifunza na kupewa mtihani au majaribio. Nyanja hii Benjamin Bloom (1956) ameigawa katikavifungu (ngazi) sita vilivyopangwa kuanzia kifungu kilicho rahisi hadi kilicho tata. Vifungu hivyo ni
Maarifa
Ufahamu
Matumizi
Uchambuzi
Uunganishaji/ uundaji
Tathimini

NGAZI YA MAARIFA
Maswali yanayoulizwa hupima uwezo wa mwanafunzi kukumbuka maarifa, stadi za jumla alilzojifunza.(Je, mwanafunzi anaweza kukumbuka alichofundishwa?). Vitenzi vinavyotumika katika maswali yanayopima ngazi hii ni kama , Taja, andika, orodhesha, eleza.
Mfano wa maswali ni kama
Taja makundi mawili ya viumbe hai
Orodhesha mambo yanayoathiri kinga ya mwli
Nini maana ya mashine?

NGAZI YA UFAHAMU
Mwanafunzi anapimwa katika ngazi hii ni kutaka kujua kama anaweza kuhusisha maarifa mapya na marifa aliokuwa nayo.(Je,mwanafunzi anaweza kukueleza nakutafsiri maana ya kitu kilichofundishwa?) Vitenzi vinavyotumika katika maswali yanayopima ngazi hii ni kama Toa, fupisha, eleza.
Mfano wa maswali ni kama
Toa tofauti kati ya wanyama na mimea.
Eleza athari za UKIMWI katika jamii.

NGAZI YA MATUMIZI
Ngazi hii huhusisha maswali yanayomtaka mwanafunzi kutumia habari anayoifahamu kupata jibu. (Je, mwanafunzi anaweza kutumia maarifa na stadi katika mazingira mapya kuhusu mambo aliyofundishwa?) Vitenzi vinavyotumika katika maswali yanayopima ngazi hii ni kama
Kokotoa mlinganyo ufuatao
2x+y= 1 na 2x-y=2
Elezea kwa ni meli inaelea juu ya maji.

NGAZI YA UCHAMBUZI
Ngazi hii mwanafunzi hutakiwa kufikiri kwa makini na maswali yanayotungwa ni yanayomtakaka mwanafunzi kuchambua maarifa na kubainisha sehemu zake na kuonyesha uhusiano.(Je, mwanafunzi anaweza kutambua na kuhusianisha sehemu mbalimbali za kitu au taarifa?).
Mfano wa vitenzi vinavyotumika ni kama kuhusianisha,changanua, gawanya,tenga.
Mfano wa maswali ni kama
Kwa nini karafuu haiwezi kustawi Lushoto?
Andika kwa kifupi kifungu cha habari kifuatacho.
Chora ramani ya Tanzania na uoneshe maziwa ma mito.

NGAZI YA UUNDAJI
Katika ngazi hii mwanafunzi hupimwa uwezo wake wa kuunganisha vitu mbalilmbali kuunda kitu kizima.(Je mwanafunzi anaweza kutoa uamuzi au kuanzisha mambo kutokana na taarifa zilizochanganuliwa?) Vitenzi vinavyotumika ni kama husianisha, jenga upya, pangilia, unda fupisha. Mfano wa maswali ni kama
Hatua gani zichukuliwe ili kupunguza matatizo kwenye utafiti?
Eleza namna utakavyoboresha mazingira yaliyoharibika kwa ajili ya ukataji miti.

NGAZI YA TATHMINI
Katika ngazi hii mwanafunzi anatakiwa kutathmini uzuri au ubaya wa matumizi ya kitu fulani na kufanya maamuzi.(Je,mwanafunzi anaweza kuamua kitu kina thamani gani au kinafaa au hakifai kufuatana na kipimo sanifu kuchunguza sifa za kitu hicho). Vitenzi vinavyotumika ni kama hakiki, hitimisha, kubaliana, tetea, toa ufupisho, toa makosa.
Mfano wa naswali ni kama
Elimu ni bora kuliko mali. Je, unakukbaliana na usemi huu? Eleza jibu lako.
Fafanua kauli hii kwa kutumia hoja tano. Utafiti wa matumizi ni bora zaidi kuliko utafiti wa msingi.
Steven Georges’ property

NYANJA YA MWELEKEO
Ni nyanja ya malezi ya hisia ambayo inahusika katika kupima tabia ya mwelekeo na mwenendo wa mwanafunzi. Lengo ni katika kujua; usafi, ushirikiano, uvumilivu juhudi na kujadili mambo.
NGAZI ZA NYANJA YA MWELEKEO
Ngazi ya kuwa tayari kupokea mambo mbalimbaali
Ngazi ya kushiriki/ kuitikia
Ngazi ya kutathmini na kuhusianisha
Ngazi ya msimamo/ Ngazi ya kuoanisha maswala mbalimbali
NGAZI YA KUWA TAYARI
Hii ni ngazi ya kwanza ambayo huonesha utayari alionao mwanafunzi kujifunza.(Je, mwanafunzi yuko tayari kupokea kichokoo,kwa mfano kukubali kushauriwa?). Vitenzi vinavyotumika ni kama chagua jibu sahihi, elekeza, fuata.
Mfano wa maswali ni kama
Utakapochelewa kipindi cha ualimu utafanya nini?
Uko tayari kusoma na mwanafunzi mlemavu
NGAZI YA KUITIKIA / KUSHIRIKI
Katika ngazi hii mwanafunzi yuko tayari kujifunza, kuonyesha mwitikio alionao kama kwa kuwa mchangamfu muda wote.(Je, mwanafunzi anaweza kushiriki katika shughuri mbalimbali yaani kuchangia mawazo na utendaji?) Vitenzi vinavyotumika ni kama amkia, saidia tambulisha, simulia, nyumbulisha . Mfano wa maswalli ni kama
Utamsaidiaje mtu alieumwa na nyoka?
Ngoma zinapochezwa usiku zinachochea maambukizi ya UKIMWI. Jadili
NGAZI YA KUTHAMINISHA
Mwanafunzi hupimwa jinsi gani anavyojisamini yeye mwenyewe, anavyothaminiwa na wenzake walimu wake na jami ikwa jumla.(Je mwanafunzianaweza kuthamini kitu wazo na watu yaani kuwajibika?) Vitenzi vinavyotumika ni kama fanya kazi, toa taarifa, shirikiana, pendekeza, pambanua.
Mfano wa maswli ni kama.
Badili asilimia kuwa desimali
Oanisha maneno kwenye orodha A nay ale yalioko kwenye orodha B.
KUOANISHA MASWALA MBALIMBALI
Mwalimu hupima uwezo wa mwanafunzi katika kulinganisha na kutofautisha vitu mbalimbali.(Je,mwanafunzi anaweza kuwa na msimamo wa fikra?) Vitenzi vitumikavyo ni kama; Unda, zingatia, husianisha tayarisha unganisha, linganisha.
Mfano wa maswali ni kama
Binadamu wote ni sawa thibitisha kauli hii.
KUWA NA MSIMAMO
Mwalimu kupima msimamo wa wanafunzi juu ya maamuzi ya maswala mbalimbali
NYANJA YA STADI
Kipengele hiki hupimwa kwenye vitu vinavyohusu utumiaji wa mikono,miguu, na sehemu nyingine za mwli. Vitu muhimu vinavyoangaliwa ni kama uwezo wa
Kutumia vifaa au zana
Kuchagua vifaa au zana muafaka
Kutunza au kurudisha vifaa/zana mahali pake
Kupata matokeo mazuri au zao bora
Nyanja ya stadi imegawanyika katika ngazi kuu tatu ambazo ni
Kuchunguza
Kuiga
Kurekebisha
KUCHUNGUZA
Je, mwanafunzi anaweza kuangalia na kusikiliza kwa makini kinachotendeka?
KUIGA
Je, mwanafunzi anaweza kkufuatisha maelekezo kwa vitendo ili kujenga mazoezi ya utendaji?
KUREKEBISHA
Je mwanafunzi anaweza kutumia misingi ya utendaji kubuni kitu kipyaau utendaji mpya?
Steven Georges’ property
ZANA ZA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Zana kuu zinazotumika katika upimaji wa maendeleo ya elimu ni pamoja na mazoezi, mitihani, muongozo wa usaili,majaribio na jedwali la kupima tabia na mwenendo wa wanafunzi.
MAZOEZI
Unapokuwa unafundisha kwa njia shirikishi ni jambo la kawaida kuwauliza wanafunzi wako maswali. Maswali haya huwa ni sehemu ya mazoezi ya kujenga somo. Vilevile hukupa mwanga ni mwanafunzi gani anafuatana na wewe unavyofundisha. Si kila mwanafunzi atapata nafasi ya kujibu maswali, njia hii haitoshi kupima ufundishaji.Ili kufanya ikamilike inabidi utoe zoezi kila amalizapo dhana,mada au sura.
MAJARIBIO
Majaribio ni mazoezi yanayotolewa na mwalimu kwa mwanafunzi ili kumpima mafanikio yao katika kujifunza. Majaribio hufanyika kuwapima wanafunzi katika mada kuu au mada nyingi.Majaribio haya hufanywa mara moja kwa kila majuma mawili, mwezi au nusu mhula, Njia hii huweza kumpima mwanafunzi anavyoendelea kupokea na kuhifadhi taaluma.
MITIHANI
Mitihani hutolea kwa shule za msingi, sekondali, vyuoni mwishoni mwa mhula. Matokeo ya mitihani huonyesha mwanafunzi anavyoendelea katika masomo yake mbalimbali iklinganishwa na wenzake.
Mitihani mikuu inayofanyika ni pamoja na
Mtihani wa kualilza darasa la saba ambao hutumika kuchagua wanafunzi kuingia sekondari kikdato cha kwanza.
Mtihani wa kidato cha pili.
Mtihani wa kkumaliza kidato cha nne ambao hutumika kuchagua wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na watakao fanya kozi mballimbali za kitaaalam
Mtihani wa kidato cha sita ambao hutumika kuchagua wanafunzi watakaoendelea na masomo zaidi ya sekondari ikwapo vyuo kikuu.
JEDWALI LA TABIA NA MWENENDO
Ni jukkumu la mwalimu kumlea mwanafunzi awapo shuleni. Hivyo inakubidi ujue tabia na mwenendo wake kila mara. Ili kuweza kufanya hivyo inakubidi kuwa na jedwali la kuchunguza mwenendo na tabia wa wanafunzi.
Steven Georges’ property
JEDWALI LA KUPIMA TABIA NA MWENENDO WA WANAFUNZI
GREDI
MAELEZO
Darasani
Huwahi kuingia darasani
Hufanya kikamilifu kazi anazopewa
Hushirikiana na wenzake katika masomo
Huondoka tu baada ya kumaliza kazi
Tabia nyingine.
Hutmiza majukumu anapopewa nafasi ya kuongoza wenzake
Ana heshima kwa walimu, watu wengine na wanafunzi wenzake
Anatunza usafi wa mwili wake na mavazi
Ni mwaminifu
Anafanya kazi kwa bidiii na stadi
Huonwa na wanafunzi wenzake kwa ushauri
Shughuri za ujenzi wa taifa
Hushiriki bila kinyongo katika kazi za ujenzi wa taifa, shuleni na nje ya shule
Hushirikiana na wenzake katika kukamilisha kazi iliyotolewa
Huwatia moyo wenzake katika kukamilisha kazi iliyotolewa
Mambo mengineyo
Anashiriki kikamilifu katika kukamilisha kazi aliyopewa
Anashiriki kikamilifu katika shughuri za utamaduni
Tumia A,B,C,D,E kupima mwanafunzi katika safu ya gredi
Ufunguo; A= Vizuri sana, B=Vizuri, C= Wastani, D= Dhaifu, E=Mbaya.
Wakati unapojaza jedwali unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo
Usiwe na jazba kutokana na tukio moja.Chunguza kwa muda endapo tukio limekkuudhi
Mshirikishe mwalimu mwenzako endapo anamjua zaidi mwanafunzi
Usitoe upendeleo
Steven Georges’Property
MWONGOZO WA USAILI
Upimaji kwa kusaili hufanyika ana kwa ana. Unapopata mwanafunzi mgeni na unapenda kujua uwezo wake au historia ya alikotoka unaweza kumuita na kuongea nae. Ili uhakikishe mambo yote unayoyataka kujua unayauliza ni vizuri kuandaa mwongozo wa usaili.
Mwongozo wa usaili haya ni maswali yalioorodheshwa kwa mpangilio maalum ili kuwa na mtiririko mzuri wa mawazo. Usaili huu pia huweza kutumika kuchunguza matatizo ya mwanafunzi katika kujifunza.
Steven Georges property
UTUNZI WA MAJARIBIO NA MITIHANI
Misingi ya utunzi wa majaribio na mitihani
majaribio na mitihani yana umuhimu mkubwa sana katika upimaji wa maendeleo ya wanafunzi. Yanajumuisha vitu halisi vinavyotarajiwa na mwalimu kutoka kwa wanafunzi baada ya kujifunza/ ujifunzaji.
Dhumuni kubwa la majaribio na mitihani ni
1.Hutupatia taarifa kamili na halisi kuhusu maendeleo ya mwanafunzi. Mwalimu anatakiwa kutoa majaribio na mitihani kwa wanafunzi ili kujua kile kinachotakiwa kupimwa kwa wakati ule. Mwalimu anpoazimia kutunga jaribio/ mitihani anatakiwa kufuata hatua zifuatazo.
Mwalimu anapaswa kufahamu vema mambo anayotaka kuyapima. Kitendo hicho kitakufanya ufanye uamuzi kuhusu maswali utakayo yatumia.
Maswali ya mitihani yagusie vipengele vingi vya maudhui yaliofundishwa kwa kipindi hicho.
Mwalimu aamue ni aina gani ya maswali atakayoyatumia. Kimsingi kuna aina kuu mbili za maswali, maswali ya kujieleza ambayo yanadai majibu yatolewe na mtahiniwa lakini kiwango cha usahihi wa majibu hayo yanatolewa na mtahini. Maswali haya yanataka mtahiniwa kujua kweli ya mambo mbalimbali na kuonyesha mambo yanayohusiana na yasio husiana. Utoaji wa majibu katika maswali ni kwa kutumia insha au majibu mafupi. Aina ya pili ya maswali ni maswali yakinifu. Maswali haya yanamtaka mtahiniwa kutambua jibu lililosahihi miongoni mwa majibu yaliotolewa na mtahini. Katika maswali haya mtahiniwa hana uhuru wa kuchagua majibu mengine yalio tofauti na yale yaliotolewa.
JEDWALI LA KUTAHINI
Kabla mwalimu hajaanza kutunga maswali anapaswa kutayarisha jedwali la kutahini. Jedwali la kutahini ni utaratibu unaonyesha maada za kupima na idadi ya maswali kwa kila maada. Jedwali hili huonyesha malengo yanatarajiwa kufikiwa pamoja na idadi ya maswali kwa kila maada. Jedwali hupangwa kwa safu. Safu ya kwanza upande wa kushoto huwekwa maudhui kwa kuorodhesha maada zinazopimwa. Safu inayofuata kulia huwekwa malengo ya kupimwa.
Watahini wengi hutumia mgawanyo wa bloom (1956) kuainisha stadi hizo. Hata hivyo hufungwi na utaratibu huu ikiwa somo lako haliwezi kupimwa kikamilifu kwa mgawanyo huo.unaweza kuweka utaritibu mwingine kama utaona unafaa zaidi.
Idadi ya maswali huonyeshwa katika mkato wa chumba cha maudhui kuelekea kulia na kile cha safu ya stadi zinazopimwa.
Jumla ya maswali kwa kila maada huandikwa upande wa kulia. Jummla ya maswali kwa kila ngazi ya utambuzi huandikwa kwenye mstari wa chini ya jedwali.
STADI ZA KUPIMWA
1
2
3
4
Jumla
Asilimia kwa kila
Maada za kupimwa
Maada za kupimwa
Jumlaya maswali
Asilimia kwa kila ngazi
UTAYARISHAJI WA JEDWALI LA KUTAHINI
Mambo ya kufanya wakati wakuandaa jedwali la kutahini
1.Chukua muhtasari wa somo na maandalio ya somo
2.Chunguza katika maandalio ya somo maada ambazo zimekishwa fundishwa
3.Chagua mada ambazo unaona ni muhimu zitungiwe jaribio/ mitihani kisha orodhesha mada hizo.
4.Chunguza kwa makini katika muhtasari na maandalio ya somo ya somo malengo mahsusi ya mada zinazotungiwa maswali
orodhesha malengo hayo kisha amua
i/ aina ya maswali yatakayotumika katika upimaji
ii/ idadi ya maswali yote katika mtihani
iii/ muda wa kufanya jaribio hutegemea na wingi wa mada na hali ya malengo yenyewe 5. chora jedwali la kutahini
6.jaza jedwali la kutahini kwa kufuata hatua hizi
i/ orodhesha mada zote za kutungiwa maswali.
ii/ orodhesha malengo mahususi katika safu inayofuata
iii/ Amua ngazi zipi za nyanja ipi za kupimwa zipewe umuhimu wa kupewa maswali mengi na zipi zipewe maswali machache.
UMUHIMU WA JEDWALI A KUTAHINI
I/ Linahakikisha kuwa maudhui yote yanayotakiwa kutahiniwa yanatahiniwa.
Ii/ Linahakikisha kuwa kiwango cha kuelewa maarifa , kumudu stadi za utendaji na kubadilika kwa mwelekeo wa watahiniwa kinatahiniwa
iii/ Linahahakikisha uwiano wa idadi ya maswali katika kila eneo na kila kipengele cha nyanja kinapimwa .
Mfanowa jedwali la utahini kwa somo la maarifa ya jamii darasa la tano katika nyanja ya mwelekeo
STADI ZA KUPIMWA
MADA Z KUPIMWA
MALENGO YA KUPIMWA
Kuwa tayari
kuitikia
Kutathmini
Kuwianisha maswala
Msimamo
Jumla
% kwa kila mada
Mahusiano ya jamii za Tanzania
1
2
3
15%
Mila na desturi
1
1
1
3
15%
Kufanya kazi
1
1
1
3
15%
Kusoma ramani
1
2
3
15%
Muundo wa serikali ya kijiji
2
1
3
15%
Ushiriki wa jamii
2
3
5
15%
Idadi ya maswali
5
6
2
4
3
20
15%
% kwa kila ngazi
25%
30%
10%
20%
15%
100%
100%
UCHAMBUZI WA TAFSIRI YA MATOKEO YA MAJARIBIO NA MITIHANI
Baada ya mwalmu kusahihisha jaribio / mtihani na kutoa alama hatua inayofuata ni uchambuzi wa tafsiri ya jaribio/ mtihani.
Kuna mambo mawili makubwa yanayojumuishwa ;
i.Kufanya uchanganuzi na tafsiri ya takwimu ya maksi (alama) inayokusudiwa kutathimini kiasi cha mafanikio ya utendaji wa mtahiniwa.
ii.Kufanya uchanganuzi wa maswali ya jaribio ili kuona iwapo jaribio lilitumika kupima ufanisi wa utendaji wa watahiniwa katika nyanja mbalimbali za kujifunza lilifaa kwa kiasi gani.
UCHAMBUZI WA MATOKEO YA MTIHANI NA TAFSIRI
Uchambuzi wa matokeo ni mchakato mzima wa kurekodi kuzipanga alama kulingana na mahitaji ya mtumiaji .
MADHUMUNI YA KUCHAMBUA
Kuelewa ujuzi uliotarajiwa kujengwa na mwanafunzi kama ilivyokusudiwa.
Kupima mafanikio ya kazi ya mwalimu.
UMUHIMU WA KUCHAMBUA NA KUTAFSIRI DATA
Inamsaidia mwalimu kujitathimini mwenyewe katita utendaji wa kazi
Inamsaidia mwalimu kufahamu viwango vya ujuzi walionao wanafunzi
Inamsaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya mbinu na njia za kufundishia
Inamsaidia kupanga mikakati ya kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kujifunza
Inasaidia wanafunzi kujitathimini wao wenyewe kwa kufahamu maeneo wanayoyamudu na wasiyoyamudu.
Inatoa nafasi kwa jamii kuelewa/kufahamu jinsi ya kufanya marekebisho juu ya mitaala.
Istilahi zinazotumika katika kuchambua matokeo ya mitihani ni ukokotoaji wa :Wastani, modi, mfiko alama yakati (mediani ).
Wastani
Wastani ni kiwango cha kati cha hesabu.
Hupatikana kwa kujumlisha maksi zote halafu kugawanya kwa idadi ya watahiniwa.
i.e
Wastani = Jumla ya alama
Idadi ya watahiniwa
Endapo alama zimetolewa kwa jedwali la marudio, idadi ya watahiniwa ni
X=∑fx/∑f
Mfano 12,24, 36, 25.
Alama
Chale
Marudio
fx
67
1
1
67
66
1
1
66
64
1
1
64
61
1
1
61
55
11
2
110
45
1
1
45
35
1
1
35
27
1
1
27
25
1
1
25
Dosari za alama za wastani
Haituelezi ubora au ufanisi wa kujifunza na maendeleo ya wanafunzi.
Manufaa ya alama ya wastani
Hutumika kutafuta ukatikati wa maendeleo ya mwanafunzi.
Hutusaidia kutupa picha ya maendeleo ya mwanafunzi ikiwa idadi ni kubwa.
MODI
Modi ni alama iliyojitokeza mara nyingi kupita alama nyingine. Ni alama yenye marudio (f) mengi zaidi.
Mfano 23,33,24,24,32,25,22,24,26 na 25.
modi yaweza kuwa ni namba moja au zaidi ya moja endapo marudio yanalingana au hakukua na alama zisizojirudia.
MFIKO
Mfiko ni tofauti iliyopo kati ya alama ya juu kabisa na alama ya chini kabisa katika seti ya maksi za watahiniwa. Mfano
tafuta mfiko kwa alama zifuatazo
73,35, 42, 85, 36 na 78
Mfiko = 85-35=50
Endapo mfiko (range) ni ndogo, tafsiri yake ni kuwa watahiniwa walikuwa nauwezo uliokaribiana au unaokaribia kulingana.
Endapo mfiko ni mkubwa hiyo inaonyesha kuwa watahiniwa wana uwezo tofauti, yaani wapo wenye uwezo wa juu zaidi na wapo wenye uwezo wa chini zaidi.
UWEZO WA SWALI KUPAMBANUA
Katika upimaji, swali zuri ni lile ambalo wanafunzi walio hodari wenye uelewa na ujuzi wa kiwango cha juu zaidi kitaaluma watalifanya vizuri na wale wenye kiwango cha chini zaidi kitaaluma wtalifanya vibaya.
Hii ina maana kuwa swali zuri(pamoja na sifa au vigezo vingine) ni lazima liwe na uwezo wa kupambanua wanafunzi walio hodari na wasio hodari.
Namna ya kukokotoa uwezo wa swali kupambanua
1. Panga wanafunzi kuanzia alama za juu hadi za chini
2.Gawa watahiniwa katika makudi matatu. H: maksi za juu (1⁄3N), kundi la kati (1⁄3N) na L. maksi za chini (1⁄3N).
sampuli ya uchanganuzi ambayo hasa ndio inayohusika na ukokotozi wa upambanuzi wenyewe huitwa T, nayoundwa na kundi la Juu la H na lile la chini L.
T= H+L
3.Kokotoa uwezo wa kupambanua (D) kwa kutumia kanuni hii
D =RH-RL⁄½T
Wakati D= ni uwezo wa swali kupambanua
RH= ni idadi ya H waliopatwa swali.
RL= ni idadi ya L waliopatwa swali
T= ni idadi ya walioshirikishwa. Kundi shiriki ambalo ni (1⁄3N) ya juu na (1⁄3N) wa chini
mfano wa ukokotozi.
Kwenye mtihani uliofanywa na wanfunzi 18, wanafunzi 4 bora walipata swali la tano na wanfunzi 2 duni walipata swali hilo.
Kutoka kwenye kanuni
D =RH-RL⁄½T
H= 1/3* 18= 6
L= 1/3* 18= 6
T= H+L=12
D= (4-2/½*12)= 2/6
D= 0.3
Kwa hiyo kiwango cha ugumu wa swali mla 5 D5= 0.3.
unapopata D= +1; hii ni namba ya juu kabisa. Namba hii tafsiri yake ni kuwa wanafunzi wote hodari wamelipata swali na wasio hodari wamelikosa.
Ukipata D= 0 hii ina maana kuwa swali husika halina uwezo wowote wa kupambanua.
Endpo D=-1 tafsiri yake ni kuwa wa wanafunzi wengi wenye uwezo wa chini wamelipata swali hilo ukilinganisha na wanafunzi wenye uwezo wa chini. Swali au maswali kama hayo hayafai kwenye mtihani.
Mwongozo wakutambua maswali ya mtihani yalio bora
Kiwango cha D
Tafsiri yake
Uamuzi wa kuchukua
0.4 na zaidi
Swali linafaa
Libaki katika mtihani
0.2- 0.39
Haliridhishi
Lilekebishwe kisha lijaribiwe tena,
0.1- 0.19
Halilidhishi
Liondelewe katika mtihani
D=-(Hasi)
Halilidjishi
Liondelewe katika mtihani

Kwa Mabo mengine mazuri na matamu zaidi usikose kuitembelea blog yangu
AY director

Wednesday, September 13, 2017

Sheria za mwendo za NEWTON (NEWTON'S LAWS OF MOTION)

Sheria za mwendo za NEWTON (NEWTON'S LAWS OF MOTION

Jinsi sheria hizi za mwendo zisivyobadilika ndivyo na sheria za mafanikio zisivyobadilika. Bila ya kukuchosha naomba twende moja kwa moja kwenye sheria hizi tatu.

Sheria ya kwanza; Sheria ya utulivu(law of inertia)
Sheria hii inasema kitu chochote ambacho kipo kwenye hali ya utulivu kitaendelea kuwa kwenye hali hiyo kama hakuna nguvu yoyote itakayokifanya kiondoke kwenye hali hiyo. Kwa mfano ukiweka kitabu juu ya meza kitakaa hapo miaka nenda miaka rudi mpaka nguvu itakapowekwa kukiondoa au kukisukuma.

Unatumiaje kwenye mafanikio? Hivyo ulivyo utaendelea kuwa hivyo hivyo kama hutatumia nguvu yoyote kubadili hali uliyonayo sasa. Kama kila siku unaamka unakwenda kufanya kazi, unarudi unapumzika unalala utaendelea hivyo hivyo kuwa na maisha yasiyokuwa na mafanikio mpaka utakapoweka nguvu kubadili hali hiyo. Moja ya nguvu unazoweza kuweka sasa na kubadili maisha yako ni kuweka malengo makubwa na kuanza kuyatekeleza. Bonyeza hapa kujua zaidi.

Sheria ya pili; Sheria ya mwendo kasi(law of momentum)

Sheria hii inasema kitu chochote ambacho kipo kwenye mwendo kitaendelea na mwendo huo huo kama hakuna nguvu itakayowekwa kupunguza au kuongeza mwendo huo. Kwa mfano kama kusingekuwa na nguvu ya mvutano kwenye dunia, ungerusha kitu kingeenda angani na kupotea kabisa.

Unawezaje kutumia sheria hii kwenye mafanikio?

Mara baada ya kuweka malengo yako na kuanza kuyatekeleza hakikisha huachi hata siku moja kile unachofanya. Kama usipoacha utaendelea vizuri na utafikia mafanikio. Kama ukiacha itakuwa vigumu sana kwako kuanza tena kama ilivyo kwenye sheria ya kwanza. Kama umeamua kufanya mazoezi ili kuweka afya yako vizuri usiache, kama umeamua kuacha kupoteza muda endelea hivyo hivyo na lazima utafikia mafanikio makubwa.

Sheria ya tatu; vitendo(law of action and reaction)

Sheria hii inasema kwamba nguvu unayoweka kwenye kufanya kitendo ndio nguvu hiyo hiyo unayoipata kutoka kwneye kitendo hicho. Yaani kama unasukuma ukuta na ukuta nao unakusukuma kwa nguvu sawa na unayoiweka.

Unatumiaje sheria hii kwenye mafanikio?

Jinsi utakavyoweka juhudi kubwa kwenye kufikia mafanikio ndivyo utakavyopata mafanikio makubwa zaidi. Sina haja ya kuzungumzia hili sana kwa sababu tumeshalijadili sana kwneye makala mbalimbali. Kama ukifanya kazi/biashara kawaida na wewe utaishia kuwa wa kawaida. Kama ukifanya kazi/biashara kipekee utakuwa wa kipekee. Kile unachoweka ndio unachopata.

Kumbuka sheria hizi tatu kila siku ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

1. Kama hupendi hali uliyonayo sasa ibadili, na sio kuilalamikia.

2. Ukianza kufanya jambo endelea kulifanya, usikate tamaa wala kuishia njiani.

3. Kama unataka kupata mafanikio makubwa, weka juhudi kubwa kwenye kazi au biashara yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kutengeneza mafanikio makubwa sana.
Asante sana karbu tena kwenye Blog yangu AY BALEMBA

Tuesday, August 15, 2017

How Simple is Life?

  Lessons from “The Boy Who Harnessed the Wind”

You’ve probably never heard of William Kamkwamba, but his life story is one you should know. William dropped out of school in rural Malawi when he was 14 because his family couldn’t afford to pay his fees. He then sat at home for 6 years.

One day, he found a book in the local library describing how a windmill generates electricity. Using only the pictures in the book, William figured out how to build his own windmill using scrap metal, pipes, wooden planks and an old bicycle dynamo he found in the village. People thought he had lost his mind--what on earth was he doing collecting all those scraps ?

But guess what, he managed to generate electricity from his windmill! Before you knew it, everyone in the village was coming to his house to charge their cellphones and radios, and he became the hero who transformed the lives of his fellow villagers.

Inspired by his story, we admitted WIlliam into the first ever class of African Leadership Academy 10 years ago. He could hardly speak English and was several years behind his classmates, even though he was much older. Our team at ALA helped him catch up and gain admission to an Ivy League university in the USA (Dartmouth). He’s since gone on to become a global phenomenon. He published a book (“The Boy who Harnessed the Wind”) which became an Amazon bestseller, gave a Ted Talk, and has appeared on The Daily Show, CNN and Good Morning America. He’s transformed his entire village by building a school that has over 400 students, and has brought clean drinking water and electricity to several hundred people in the village.

William  has taught me 3 key lessons  I always come back to :

1.__Use what you have until you get what you need
William is today seen as an engineering genius, but he didn’t always have what he needed to make the things he wanted to make. He didn’t have a fancy laboratory or even electricity. But he used what he had around him- scrap metal, to achieve his goal. If you want to be a photographer but can’t yet afford a camera, maybe start by taking photos with your phone. The most important thing is not the materials or equipment you have, but to practice your craft and hone your skills. The fancy labs, equipment, laptops, cameras etc will come later. 

2.__Take criticism to your head and not to your heart
Some people in William’s village  looked at him collecting scraps and thought he had gone crazy. If you have big dreams, many people will criticize you and be skeptical about whether your ideas will succeed. That’s ok---remember that if you’re doing something people have not seen before, they may not understand your vision or see what you see. Listen to criticism if it’s constructive, but avoid being discouraged by pure negativity. People will come around when they start to see the results of your work. 

3.__Innovation is right where you are if you pay attention
Look around you and observe your environment very carefully. What problems do you see? What can be improved? Many times, the things that improve our lives (what many people call innovations)  come from making simple observations and designing a solution that addresses the challenges you see. So don’t wait for others to solve the problems in your society. Use your creativity to think of solutions. You never know what exciting innovations lie in your head until you try.

What problems do you see around you? What simple things that you may take for granted can you can use to build a solution? What’s your version of William’s windmill and how will you build it?

Nyanja za ujifunzaji na mifano yake. (Robert Gagne)





This theory stipulates that there are several different types or levels of learning. The significance of these classifications is that each different type requires different types of instruction. Gagne identifies five major categories of learning: verbal information, intellectual skills, cognitive strategies, motor skills and attitudes. Different internal and external conditions are necessary for each type of learning. For example, for cognitive strategies to be learned, there must be a chance to practice developing new solutions to problems; to learn attitudes, the learner must be exposed to a credible role model or persuasive arguments.

Gagne suggests that learning tasks for intellectual skills can be organized in a hierarchy according to complexity: stimulus recognition, response generation, procedure following, use of terminology, discriminations, concept formation, rule application, and problem solving. The primary significance of the hierarchy is to identify prerequisites that should be completed to facilitate learning at each level. Prerequisites are identified by doing a task analysis of a learning/training task. Learning hierarchies provide a basis for the sequencing of instruction.

In addition, the theory outlines nine instructional events and corresponding cognitive processes:

1.Gaining attention (reception)
2.Informing learners of the objective (expectancy)
3.Stimulating recall of prior learning (retrieval)
4.Presenting the stimulus (selective perception)
5.Providing learning guidance (semantic encoding)
6.Eliciting performance (responding)
7.Providing feedback (reinforcement)
8.Assessing performance (retrieval)
9.Enhancing retention and transfer (generalization).

These events should satisfy or provide the necessary conditions for learning and serve as the basis for designing instruction and selecting appropriate media (Gagne, Briggs & Wager, 1992).

Application

While Gagne's theoretical framework covers all aspects of learning, the focus of the theory is on intellectual skills. The theory has been applied to the design of instruction in all domains (Gagner & Driscoll, 1988). In its original formulation (Gagne, 1 962), special attention was given to military training settings. Gagne (1987) addresses the role of instructional technology in learning.

Example

The following example illustrates a teaching sequence corresponding to the nine instructional events for the objective, Recognize an equilateral triangle:

1. Gain attention - show variety of computer generated triangles
2. Identify objective - pose question: "What is an equilateral triangle?"
3. Recall prior learning - review definitions of triangles
4. Present stimulus - give definition of equilateral triangle
5. Guide learning- show example of how to create equilateral
6. Elicit per formance - ask students to create 5 different examples
7. Provide feedback - check all examples as correct/incorrect
8. Assess performance- provide scores and remediation
9. Enhance retention/transfer - show pictures of objects and ask students to identify equilaterals

Gagne (1985, chapter 12) provides examples of events for each category of learning outcomes.

Principles

Different instruction is required for different learning outcomes.
Events of learning operate on the learner in ways that constitute the conditions of learning.
The specific operations that constitute instructional events are different for each different type of learning outcome.
Learning hierarchies define what intellectual skills are to be learned and a sequence of instruction.
References

Gagne, R. (1962). Military training and principles of learning. American Psychologist, 17, 263-276.

Gagne, R. (1985). The Conditions of Learning (4th.). New York: Holt, Rinehart & Winston.

Gagne, R. (1987). Instructional Technology Foundations. Hillsdale, NJ: Lawrence Erlbaum Assoc.

Gagne, R. & Driscoll, M. (1988). Essentials of Learning for Instruction (2nd Ed.). Englewood Cliffs, NJ: Prentice-Hall.

Gagne, R., Briggs, L. & Wager, W. (1992). Principles of Instructional Design (4th Ed.). Fort Worth, TX: HBJ College Publishers.
Asante karibu Tena

Thursday, August 3, 2017

YAJUE MAISHA YA MWANASAIKOLOJIA JEAN PIAGET @AY De Balemba

GEAN PEAGET

Jean Piaget (French: [ʒɑ̃ pjaʒɛ]; 9 August 1896 – 16 September 1980) was a Swiss clinical psychologist known for his pioneering work in child development. Piaget's theory of cognitive development and epistemological view are together called "genetic epistemology".



Born    9 August 1896
Neuchâtel, Switzerland
Died    16 September 1980 (aged 84)
Geneva, Switzerland
Fields    Developmental psychology, epistemology
Alma mater    University of Neuchâtel
Known for    Constructivism, genetic epistemology, theory of cognitive development, object permanence, egocentrism
Influences    Immanuel Kant, Henri Bergson,[1] Pierre Janet, Alfred Binet, Théodore Simon, James Mark Baldwin[2]
Influenced    Bärbel Inhelder,[3] Jerome Bruner,[4] Kenneth Kaye,[citation needed] Lawrence Kohlberg,[5] Robert Kegan,[6] Howard Gardner,[7] Thomas Kuhn,[8] Seymour Papert,[9] Lev Vygotsky[10][11]
Piaget placed great importance on the education of children. As the Director of the International Bureau of Education, he declared in 1934 that "only education is capable of saving our societies from possible collapse, whether violent, or gradual."[12] Piaget's theory and research influenced several people. His theory of child development is studied in pre-service education programs. Educators continue to incorporate constructionist-based strategies.

Piaget created the International Center for Genetic Epistemology in Geneva in 1955 while on the faculty of the University of Geneva and directed the Center until his death in 1980.[13] The number of collaborations that its founding made possible, and their impact, ultimately led to the Center being referred to in the scholarly literature as "Piaget's factory".[14]

According to Ernst von Glasersfeld, Jean Piaget was "the great pioneer of the constructivist theory of knowing."[15] However, his ideas did not become widely popularized until the 1960s.[16] This then led to the emergence of the study of development as a major sub-discipline in psychology.[17] By the end of the 20th century, Piaget was second only to B. F. Skinner as the most cited psychologist of that era.[18]

Personal life   

Piaget was born in 1896 in Neuchâtel, in the Francophone region of Switzerland. He was the oldest son of Arthur Piaget (Swiss), a professor of medieval literature at the University of Neuchâtel, and Rebecca Jackson (French). Piaget was a precocious child who developed an interest in biology and the natural world. His early interest in zoology earned him a reputation among those in the field after he had published several articles on mollusks by the age of 15.[19]

He was educated at the University of Neuchâtel, and studied briefly at the University of Zürich. During this time, he published two philosophical papers that showed the direction of his thinking at the time, but which he later dismissed as adolescent thought.[20] His interest in psychoanalysis, at the time a burgeoning strain of psychology, can also be dated to this period. Piaget moved from Switzerland to Paris, France after his graduation and he taught at the Grange-Aux-Belles Street School for Boys. The school was run by Alfred Binet, the developer of the Stanford–Binet Intelligence Scales, and Piaget assisted in the marking of Binet's intelligence tests. It was while he was helping to mark some of these tests that Piaget noticed that young children consistently gave wrong answers to certain questions. Piaget did not focus so much on the fact of the children's answers being wrong, but that young children consistently made types of mistakes that older children and adults did not. This led him to the theory that young children's cognitive processes are inherently different from those of adults. Ultimately, he was to propose a global theory of cognitive developmental stages in which individuals exhibit certain common patterns of cognition in each period of development. In 1921, Piaget returned to Switzerland as director of the Rousseau Institute in Geneva. At this time, the institute was directed by Édouard Claparède. Piaget was familiar with many of Claparède's ideas including that of the psychological concept 'groping' which was closely associated with "trials and errors" observed in human mental patterns.[21]

In 1923, he married Valentine Châtenay; the couple had three children, whom Piaget studied from infancy. From 1925 to 1929 Piaget was professor of psychology, sociology, and the philosophy of science at the University of Neuchatel.[22] In 1929, Jean Piaget accepted the post of Director of the International Bureau of Education and remained the head of this international organization until 1968. Every year, he drafted his "Director's Speeches" for the IBE Council and for the International Conference on Public Education in which he explicitly addressed his educational creduo.

Having taught at the University of Geneva and at the University of Paris, in 1964, Piaget was invited to serve as chief consultant at two conferences at Cornell University (March 11–13) and University of California, Berkeley (March 16–18). The conferences addressed the relationship of cognitive studies and curriculum development and strived to conceive implications of recent investigations of children's cognitive development for curricula.[23]

In 1979 he was awarded the Balzan Prize for Social and Political Sciences.

He was buried with his family in an unmarked grave in the Cimetière des Rois (Cemetery of Kings) in Geneva. This was as per his request
Asante kwa kutembelea blog ya Kisayansi zaidi karibu tena na tena @AY De Balemba

Wednesday, August 2, 2017

LITAMBUE SIKIO LAKO NA JINSI YA KUTIBU MATATIZO YA SIKIO @AY, Abas


Sikio  limegawika katika sehemu tatu kuu. Sehemu ya nje ya sikio, sehemu ya kati ya sikio na sehemu ya ndani ya sikio.


Kuna aina mbili ya matatizo ya masikio nayo ni:
i. Otitis media : ambayo hutokea katika sehemu ya kati ya sikio na mara nyingi huwatokea watoto wachanga na watoto wadogo.
ii. Otitis externa: ambayo hutokea katika sehemu ya ndani ya sikio na mara nyingi huwatokea waogeleaji, na hutokea zaidi wakati wa baridi.
Ishara za Matatizo ya masikio kwa Otitis media:
i. Kuumwa na kuchomwa kwa sikio
ii. Kutokwa na uchafu ndani ya sikio
iii. Kutosikia kwa ghafla
iv. Homa
Sababu za Otitis media:
Sababu kubwa ya maradhi hayo ni kuziba kwa bomba la sikio(Eustachiantube), kutokana na baridi, allergy pamoja na kuingia takataka. Hii inababisha maji maji ya sikio kujaa maji hayo nayo husababisha uvimbaji wa (ear drum) sikio.
Sababu za Otitis externa:
Hii husababishwa na baketeria au fungi, maji maji yanayoingia ndani ya sikio ndio sababu kuu ya kufanya bakteria na fungi kuzaana pia Skin allegies husababisha maradhi hayo.
Na sababu nyengine ni ulaji mbovu wa chakula pamoja na upungufu wa usafi wa mwili .

DAWA ZA KUJITIBU MARADHI YA MASIKIO:
i. Nyunyiza juisi ya Kitunguu saumu katika sikio linalouma
ii.v Nenda Hospitali ukapigwe bomba ili maji na uchafu upate kutoka
iii. Pasha moto mafuta ya Zaituni (Olive oil) na yasubiri yapowe na ujitie drops mbili hadi 3
iv. Na usafishe masikio yako kila baada ya kutoka kukoga.

KUTOKWA NA USAHA SIKIONI:
Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.
TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:
Kanuni ya kwanza:
Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili:
Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu..
Kanuni ya tatu:
Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili.
Kanuni ya nne:
Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu,
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG hii, kwa Elimu zaidi Karibu tena
@AY, Abas Yusuph: De BALEMBA

Tuesday, August 1, 2017

HATUA ZA MAKUZI YA MTOTO. @AY, Abas


Hivi umeshawahi kujiuliza hata siku moja, kwa nini watu wengine ni walevi? Wengine waongeaji sana? Wengine wakimya sana? Wengine waongo sana? Wengine wana tamaa ya ngono kupita kiasi na kadhalika? Lakini pengine una maswali mengi ya namna hii ambayo yanaonyesha jinsi wanadamu wanavyotofautiana.
Kuna hatua 5 muhimu ambazo mtoto lazima afanye mambo ambayo yanastahili kufanyika katika hatua husika. Na iwapo hayatafanyika, hali hizo huhifadhiwa katika mawazo yake ya kina na hivyo kumsababishia matatizo makubwa ukubwani.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-
 1.Hatua ya kwanza – oral stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia siku moja mpaka miaka miwili. Katika hatua hii ya kwanza, furaha na raha ya mtoto huwa imejificha mdomoni. Utakuta mtoto kila wakati anafurahia kunyonya maziwa ya mama yake, vidole au midoli. Mtoto anatakiwa atumie mdomo wake mpaka ile hamu yake yote iishe. Kama ni kunyonya basi aendelee kufanya hivyo mpaka pale utakapofika wakati mzuri wa kumwachisha ziwa. Kumnyanyasa mtoto wakati ananyonya au kumfanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana ikiwa ni pamoja na kumwachisha ziwa mapema, husababisha hamu yake ya kuutumia mdomo ibaki na hivyo kuhifadhiwa kwenye mawazo yake ya kina. Anapokuwa mtu mkubwa hulipa kisasi bila kujua kwa kuutumia mdomo kwa kadri anavyoweza. Hivyo anapokuwa mtu mkubwa anaweza akawa muongo sana, mlevi kupindukia, mvuta sigara sana, muongeaji sana, au mmbeya sana. Kama kuna watu unawafahamu wenye tabia hizi, jaribu kupeleleza kama walinyonyeshwa bila kunyanyaswa au kama hamu yao ya kunyonya iliisha.

2.Hatua ya pili – anal stage: Hatua hii humhusu mtoto wa miaka miwili au mitatu. Matumizi ya mdomo huwa yamekwisha na raha huhamia sehemu za haja. Katika hatua hii, mtoto hupendelea zaidi kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara. Katika kipindi hiki wazazi wengi hufanya makosa. Mzazi anashauriwa kuwa makini kwa kutoa mafunzo mazuri kwa mtoto wake, kumfundisha jinsi ya kujisaidia au jinsi ya kutumia choo. Kinyume na hivyo ni kumfanya mtoto awe na tabia ya kujifanyisha na hivyo kuwa na hali mbaya ukubwani. Mtoto aliyenyimwa huduma hii akiwa katika hatua hiyo hubakiwa na deni, anapokuwa mkubwa anaweza kupata matatizo ya kiakili. Watoto waliokosa huduma hiyo wanapokuwa wakubwa, mara nyingi huwa mashoga, na wengine huwa waoga kufanya mapenzi, lakini mbaya zaidi ni kukosa kabisa hamu ya mapenzi, wengine huwa wazembe na huwa na tabia fulani fulani ambazo zinahitaji msaada mkubwa wa wengine.

3.Hatua ya tatu – phallic stage: Hatua hii huwahusu watoto wenye umri wa miaka minne. Ni katika hatua hii ambapo mtoto huanza kutambua jinsia yake na hivyo kuwa karibu na mama yake au baba yake. Mtoto wa kiume hupenda kulala na mama yake na mtoto wa kike pia huwa hivyo hivyo hupenda kulala na baba yake (interest of opposite sex). Mtoto wa kiume humchukia baba yake bila kujua na kumuonea wivu mama yake na kuona kama anamfaidi baba yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake, pia mtoto wa kike humchukia baba yake na kumuonea wivu baba yake na kuona kama anamfaidi mama yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake. Watoto waliokosa kuwa karibu na wazazi wao wa jinsia tofauti katika hatua hii, wengi hupata matatizo, lakini hulipiza kisasi kwa sababu hawakuwa karibu na jinsia tofauti wanapohitaji kufanya hivyo. Usishangae kumkuta binti akiwa kwenye kundi la wavulana au mvulana akiwa kwenye kundi la wasichana.

4.Hatua ya nne – latency stage: Hatua hii huwahusu watoto wa miaka sita, minane na wakati mwigine mpaka miaka 12, ambapo mtoto macho yake yote huwa katika michezo ya kawaida na kwenda shule. Hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika hatua hii kati ya jinsia ya kike na ya kiume.

5.Hatua ya tano - genital stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia miaka 13. katika kipindi hiki vijana wengi huanza kubalehe na kuvunja ungo. Katika hatua hii ndipo mtu hukabiliwa na vitu vingi katika maisha yake yote. Huanza kujishuhulisha na kutafuta maisha yake mwenyewe na ndipo hatua nyingine zote huanza kujirudia tena kama hazikufanywa vizuri katika umri huo. Raha ya mwanadamu yoyote katika kipindi hiki huwa ni mapenzi, lakini hutofautiana kiwango cha kupenda au kutamani kutokana na jinsi alivyolelewa katika hatua nne za mwanzo. Nakuomba sana kila unapokutana na watu waongo, wambeya, wakimya, wapenda ngono kupita kiasi n.k. waulize maisha yao ya utZAIDI. @AY, De Bakemba
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YANGU KARBU TENA KWA ELIMU ZAIDI