Monday, January 15, 2018

KANUNI ZA KUTAFUTA MAENEO YA NYUSO ZA MAUMBO YA UKUMBI.

KANUNI ZA KUTAFUTA MAENEO YA NYUSO ZA MAUMBO YA UKUMBI.    Ay director

NA.UMBO/MCHOROKANUNI
1.Mche mstatili.
formula20
Eneo la mche mstatili.
Eneo = (ur. \times up. \times 2) + (ur. \times h \times 2) + (up. \times h \times 2)
ur. = urefu, \;\; up. = upana, \;\; h = kimo
2.Mche duara ulio wazi pande zote.
formula17
Eneo la mche duara ulio wazi pande zote.
Eneo = 2 \pi rh \;\; AU \;\; Eneo = \pi dh
\pi = \frac{22}{7}, \; \; r = \frac{1}{2}kipenyo, \; \; d = kipenyo.
3.Mche duara uliozibwa upande mmoja.
formula19
Eneo la mche duara uliozibwa upande mmoja.
Eneo = 2 \pi rh + \pi r^2 \;\; AU \;\; Eneo = \pi dh + \frac{\pi d^2}{4}
\pi = \frac{22}{7}, \; \; r = \frac{1}{2}kipenyo, \; \; d = kipenyo.
4.Mche duara uliozibwa pande zote.
formula18
Eneo la mche duara uliozibwa pande zote.
Eneo = 2 \pi rh + 2 \pi r^2 \;\; AU \;\; Eneo = \pi dh + 2 \frac{\pi d^2}{4}
\pi = \frac{22}{7}, \; \; r = \frac{1}{2}kipenyo, \; \; d = kipenyo.
5.Mche pembetatu.
formula13
Eneo la mche pembetatu.
Eneo = [E \Delta (ABE) \times 2 ]+ [E(ABCF) \times 2] + [E(AEDF) \times 2] + [E(EBCDE)\times 2]
5.Mche mraba.
formula22
Eneo la mche mraba.
Eneo = (Up. \times Up. \times 6)
Up. = upande

Wednesday, November 22, 2017

Dhana ya Tamithiliya. AY director


TAMTHILIYA

Kwa kuanza na maana ya tamthiliya imeelezwa na wataalamu mbalimbali kwa namna tofautitofauti kulingana na vigezo walivyovizingatia.
Mwenda Ntarangwi, (2002:169) anaeleza kuwa, neno tamthilia limetokana na kitendo “mithilisha” ambacho maana yake ni kufananisha au kumithilisha hali ya maisha fulani kwa vitendo. Akahitimisha kwa kusema tamthilia ni maigizo ya matukio au visa fulani kwa uhalisi wake kwa ajili ya kuyasawili maudhui au maelezo fulani. Ubora unaojitokeza katika maana hii ni kuzingatia vipengele vya uigizaji, tukio, suala la kuhusianisha na jamii na kubeba maudhi Fulani.
Udhaifu wa maana hii ni kutozingatia kipengele cha ubunifu pia hakueleza hayo maigizo yanatakiwa yawe ya namna gani ili yaitwe tamthiliya.
 Wamitila, (2002:7) ameeleza kuwa, neno tamthiliya kwa upana wake linatumiwa kujumuisha maneno drama na
play ya Kiingereza. Kwa hiyo, tamthiliya ni utungo unaoandikwa kwa mtindo wa mazungumzo. Ubora wa fasili hii imezingatia kipengele cha mazungumzo ambacho ni kipengele muhimu katika tamthiliya.
Udhaifu wa fasili hii kwanza amechanganya dhana ya tamthiliya na drama ambazo ni dhana mbili tofauti. Kwani tamthiliya msisitizo wake upo katika maandishi lakini drama msisitizo wake upo katika uigizwaji jukwaani. Pia si kila mazungumzo ni tamthiliya. Kigezo cha mazungumzo pekee hakitoshi kuamua utungo fulani kuwa ni tamthiliya.
Penina Mlama, (1983:203) akirejelewa na Mulokozi, (1996) anasema tamthiliya ni sanaa za maonyesho; sanaa ambayo huwasilishwa ana kwa ana, tukio fulani kwa hadhira kutumia usanii wa kiutendaji. Katika fasili hii Mlama amezingatia vipengele vya sanaa, uonyeshaji, hadhira, utendaji na tukio.
Udhaifu wa maana hii ni kuwa si lazima tamthiliya iigizwe jukwaani; vilevile fanani na hadhira si lazima wawe ana kwa ana. Mfano katika tamthiliya ya “Kivuli Kinaishi” “Ngoma ya Ng’wanamalundi”, “Lina Ubani” na nyinginezo, fanani na hadhira hawapo ana kwa ana.
Udhaifu wa fasili hii Mlama hakuweka wazi urefu huu kuwa ni urefu wa kurasa nyingi au urefu wa tukio linalosimuliwa. Pia si kila hadithi inayosimuliwa jukwaani ni tamthiliya. Kwani hata misikitini na makanisani wahubiri husimama juu ya mimbari kuhutubia waumini wao. Je, hiyo ni tamthiliya? Jawabu ni kuwa hiyo siyo tamthiliya.
Sanjari na hao Mulokozi, (1999:188) anasema kuwa tamthiliya au drama ni fani ya fasihi iliyokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili ya hadhira fulani. Ubora unaopatikana katika maana hii ni kwa kuwa imezingatia utendaji, jukwaa, hadhira, kusudio na fani inayotendwa. Kwa upande wa udhaifu, maana hiiimechanganya dhana ya tamthiliya na drama. Lakini kwa kiasi kikubwa maana hii inaonekana kukidhi vigezo vingi.
Tunakubaliana na Mulokozi (1996) kuwa sifa walizotoa Mlama na Balisidya kuwa tamthiliya huwa na sifa za kawaida za sanaa za maonyesho. Sifa hizo ni dhana inayotendeka, mtendaji, uwanja wa kutendea, na watazamaji. Hivyo sifa hizi hazitoshi kupambanua sanaa ya maonesho; kwa sababu kuna matendo mengine ya kijamii ambayo yana sifa hizo. Mfano matambiko, hotuba zinazotolewa na watu mbalimbali. Mulokozi alisema sanaa za maonesho ni tukio lenye sifa saba ambazo ni dhana inayotendwa, uwanja wa kutendea, watendaji, hadhira, kusudio la kisanaa, muktadha wa kisanaa na ubunifu.

Kwa jumla tunaifasili tamthiliya kuwa ni utanzu wa fasihi unaotumia lugha ya majibizano yenye ubunifu wa hali ya juu ikiwa haina msisitizo wa uwasilishaji wake jukwaaani ili kufikishalengo mahususi kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia iliyoandikwa au isiyoandikwa.
Kutokana na kuwa dhana ya tamthiliya inachanganywa na maana ya drama ni vyema tuelezee maana ya drama. Kwa mujibu wa Wamitila, (2003:36) anasema kwamba drama ni aina ya utanzu wa fasihi ambao kimsingi hudhamiriwa kuigizwa mbele ya hadira. Inaweza kuwa imeandikwa au la.
Kwa jumla dhana ya drama inarejelea utungo wa kisanaa unaotumia lugha ya majibizano na matendo yenye ubunifu wa hali ya juu yanayotendwa jukwaani mbele ya hadhira ili kufikisha lengo mahususi kwa hadhira iliyokusudiwa.

SIFA ZA TAMTHILIYA
Utoshelevu Kimuundo. Tamthiliya nzuri huwa na sehemu tatu muhimu: Mwanzo, Katikati na Mwisho. Sehemu zake zinatazamiwa kuingiliana, kujengana na kukamilishana.
Tamthiliya huwa na lengo. Katika zama za Aristotle, kwa mfano, tanzia ziliwajibika kuzindua hofu na huruma.
Vitendo vyote vinavyofanyika katika tamthiliya vinapaswa kuchangia katika ufanisi wa dhamira za mtunzi.
Kifani, tamthiliya hutumia mbinu za kisanii zinazowishi wasomaji au watazamaji kuendelea kusoma au kutazamia matokeo ya matendo yanayoigwa. Mbinu hizo ni pamoja na jazanda, kejeli, ritifaa, tashbihi, tashihisi na uzungumzi nafsia.
Wasanii bora wa tamthiliya ni wale wanaotunga tamthiliya zinazozungumzia kadhia zinazoweza kutimia katika maisha ya binadamu.

UHALISIA MAZINGAOMBWE
Uhalisia mazingaombwe ni dhana ambayo imeanza kutumika miaka ya 1920, ambapo mjerumani Franz Roh ndiye aliyevumbua matumizi ya
Magical realism mnamo mwaka 1925 ili kuelezea kazi ya mtindo wa ulaya enzi hizo. Roh alilibuni neno hili ili kuelezea michoro iliyo na uhalisi kama wa picha na kamera. Michoro hiyo ilichanganya mambo ya uhalisi na yasiyokuwa na uhalisi.Baadaye dhana hii ya Uhalisia Mazingaombwe
ilitumiwa na Arturo Urslar kutoka Venezuela alipokuwa anahakiki kazi mbalimbali za wanafasihi wa Marekani ya Kusini waliokuwa wanatumia mtindo huu katika kazi zao. Baadaye Uhalisia Mazingaombwe ulianza kutumika kama nadharia ya uchambuzi wa kazi za kifasihi.
Katika fasihi ya Kiswahili wataalamu mbalimbali wanaeleza kuwa, Uhalisia mazingaombwe ni mtindo uliokuwa ukitumika muda mrefu hata kabla ya taaluma ya uandishi. Mtindo huu ulitumika katika fasihi simulizi na baadae ukatumika katika fasihi andishi. Wanaotumia mtindo huu katika fasihi andishi wanarudia au kufufua kitu ambacho kilikuwepo zamani. (Senkoro2007:11)
Dhana ya uhalisia mazingaombwe imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;
Wamitila (2003 a:274), anaeleza kuwa ni mtindo wenye sifa za kuyaelezea matukio ya kifantasia, kiajabu, au kiuchawi kwa namna ya moja kwa moja inayofanya yaonekane ya kawaida tu.
Faustine, S akimrejelea Methew, S. (1999:267) anasema, Uhalisia Mazingaombwe ni yale mambo ambayo hutokea pale ambapo mandhari na matukio halisi yanavamiwa na jambo ambalo ni la ajabu mno na ni vigumu kuaminika.
Kwa jumla, fasili zote zimegusia uhalisia mazingaombwe kama mbinu ambayo mambo ya ajabuajabu, uchawi, na yasiyo ya kawaida kutokea sambamba na yale yaliyozoeleka katika ulimwengu halisi tuujuao na kuuishi. Katika mbinu hii mazingaombwe hujitokeza
kupitia wahusika, mandhari, motifu ya kisafari na matukio kama misingi mikuu ya uchambuzi wa nadharia hii ambamo ndani yake kumefichwa taswira, ishara na sitiari zinazohusiana na maisha ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii.
Uhalisia Mazingaombwe huwa na sifa kama vile; matukio ya kustaajabisha, motifu ya kisafari, matumizi ya taswira na ishara kwa kiasi kikubwa ambayo hujengwa kutokana na matukio, wahusika na mandhari. Vilevile mbinu hii hutumika ili kuwakilisha kitu au jambo fulani.
Athari ya mbinu hii inajitokeza katika kazi za waandishi wa mwanzo wa fasihi ya Kiswahili hasa Shaaban Robert na kazi za “Kusadikika” na “Adili na nduguze”.Katika kazi hizi masuala ya safari yanajitokeza kwa kiasi kikubwa, safari siyo jambo la ajabu katika ulimwengu halisi wa maisha japo baadhi ya masaibu yaliyowafika wasafiri waliomo katika kazi hizi ni vigumu kuyaamini katika ulimwengu halisi kwani yamefungamanishwa na uajabuajabu mno. Huo uajabu ndiyo uliofanya kazi hizi na zilizofuatia baadaye kama “ Babu alipofufuka” na “Mzingile” kudaiwa zimetumia mbinu za uhalisia mazingaombwe katika kueleza ukweli na hali ya maisha ya jamii walizokusudia waandishi wa kazi hizo
Udhaifu wa uhaalisia mazingaombwe katika kazi ya fasihi.
Kuhusisha wahusika wakuu walio na akili zisizo timamu, mwingiliano-matini uliopindukia na utambulisho wenye kutetereka.
Umefungwa kwa minyororo ya lugha, na hivyo basi hauwezi kuondoa udhaifu wa lugha katika kuweza kuwakilisha hali halisi kikamilifu.

UCHOTARAISHAJI
Uchotaraishaji au fasihi ya Kiswahili ya majaribio, ni fasihi
ambayo imechota vipengele vya fasihi simulizi ya Kiswahili na kuviweka katika fasihi andishi ya Kiswahili, kwa lengo la kuleta vionjo vipya katika fasihi ya kiafrika. Dhana ya uchotaraishaji inarejelea kufufua fasihi asili ya Kiswahili kwa kutumia mbinu na vipengele vya fasihi simulizi katika tanzu za fashi andishi kama vile riwaya, ushairi na tamthiliya.
Uchotaraishaji ulifanywa mwanzoni hapa Tanzania na waandishi maarufu wa tamthiliya ya kiswahili kama vile, Ebrahim Hussein na Penina Muhando. Ebrahim Hussein alitumia mbinu hii katika tamthiliya yake ya Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi , na Penina Muhando katika tamthiliya yake ya Lina Ubani.
Baadhi ya sifa za uchotaraishaji
ni;
Mtambaji, sifa hii hujitokeza katika fasihi ya Kiswahili ya majaribio. Katika tamthiliya ya
Lina Ubani , mbinu hii ya utambaji imejidhihirisha, pale ambapo mtambaji anasimulia hadithi ya Bibi.
Mtambaji: Paukwa
Hadhira : Pakawa
Mtambaji: Hapo zamani za siku hizi, palitokea huyo Bibi kama mnavyomuona............... …(uk 2)
Matumizi ya taswira na ishara, mbinu hii hutumiwa katika fasihi simulizi kuwasilisha wazo kwa hadhira iliyokusudiwa. Dhana hii imetumiwa katika tamthiliya ya Lina Ubani, ambapo mwandishi ametumia taswira ya
zimwi, kuashiria utawala wa mabavu wa aliyekuwa rais wa Uganda Nduli Idd Amin, kama anavyosema Mtambaji;
.......Mwisho Zimwi likaamua fujo kuzifanya asubuhi na mapema,ukingoni mwa msitu lilisimama,likapiga makelele kuteremsha ardhi.(uk 18).
Wahusika, na majina, katika tamthiliya ya Lina Ubani, wahusika waliotumiwa ni Binadamu wenye majina halisi ya kiafrika, wahusika kama Bibi, Huila, Mwana Hego, Mota pia Mhusika Zimwi ambaye katika jamii za kiafrika huashiria ubaya.
Mwingiliano wa tanzu, (utomeleaji). Mbinu hii imejitokeza katika fasihi simulizi ambapo vipengele vya fasihi simulizi huingiliana katika utumizi. Katika tamthiliya ya Lina Ubani, kuna hadithi ndani ya tamthiliya pia matumizi ya wimbo ambao umeambatanishwa na utambaji. Bibi amekaa analia kwa kuimba na kuomboleza, licha ya hivyo wimbo wenyewe uko katika lugha ya jadi ya Kiafrika na una tafsiri yake kwa Kiswahili.
Ing’oma ii sikuidaha doo ae Ngoma hii siwezi Oooh!
Woi doo ae aya
Nimemwitunda dya mele do Nisimame juu ya mlima wa Mele
Ninange main a baba do Niite baba na mama
(uk 1-3)
Mianzo na Miisho ya kifomula, hii ni sifa ya kimsingi katika hadithi za fasihi simulizi ya kiafrika ambapo fanani huanza kuhadithia kwa kuweka viashirio maalumu kwa mfano, fanani husema ;
Fanani :Paukwa
Hadhira:Pakawa
Katika tamthiliya ya Lina Ubani, mwandishi ameanza kwa kuelezea hadithi yake kwa mianzo kama ya hadithi ya fasihi simulizi,kwa mfano
Mtambaji : Paukwa
Hadhira: Pakawa
Mtambaji:
Hapo zamani za siku hizi…………………(uk-2).
Mwishoni Mtambaji amemalizia kwa kitendawili ambacho anaomba hadhira impe mji ili kumalizia hadithi yake mfano Mtambaji:
Akaa!
Mwenyewe bibi kajifia
Hadithi hakumalizia
Mkitaka nimalizie mimi
Nipeni mji
Lakini mji wenyewe
Usiwe na uvundo
Kwa sababu ubani wa uvundo
Mie siujui.

TANZIA-RAMSA
Ni tamthiliya inayochanganya vipengele vya tanzia na ramsa, hutumiwa sawa na tamthiliya za kibwege - hii ni tamthiliya ambayo inaonyesha kwamba kicheko au furaha ndiyo jibu pekee la maisha kwa watu ambao hawana imani na maisha ambayo kwayo misingi thabiti ya maisha imeondolewa. Mfano tamthiliya ya Amezidi ya S.A Mohamedi
Tanzia-ramsa ni tamthilia ambayo huonyesha mabadiliko ya aina fulani yanayogeuza mwelekeo wa matukio ya kitanzia na kuufanya kuwa tofauti au wa kufurahisha. Hali hii inaweza kupatikana kwa kuwepo kwa hasidi au mui anayetubu na kuyajutia makosa au msimamo wake au kuwepo kwa mandhari ya kiulimbwende.
Kimsingi, tanzia-ramsa ni tanzia inayoishia kwa furaha. Kinyume chake ni futuhi zimbwe. Dhana hii inaakisi kwa kiasi kikubwa baadhi ya mitazamo ya kidhanaishi ya fasihi ambapo ushujaa na tanzia havijitokezi katika hali ya kawaida kama vilivyozoeleka.
Hali hii inadhihirika katika tamthiliya kama vile ‘ The Cherry Orchard’ (Anton Chekhov, 1904), ‘ The Winter’s Tale’ (William Shakespeare, 1611).

FUTUHI/KOMEDIA (COMEDY)
Futuhi au komedia ni utungo ambao unachekesha na kuchangamsha. Tamthiliya ya aina hii inaweza kusawiria picha halisi katika maisha kwa undani ikitumia dhihaka na kejeli kwa kuchekesha. Futuhi huficha ukali wa masuto kadri inavyoendelea kuburudisha hadhira yake.
Futuhi hulenga kurekebisha tabia zinazozidhihaki au zinazozicheka. Kusema futuhi inafurahisha haina maana kuwa dhamira yake haina uzito, kwani huzungumzia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa njia ya kuchekesha. Futuhi huweza kuwa na sifa zinazotofautiana – jambo ambalo hutumiwa kama kigezo cha kuainisha aina mbalimbali. Lakini vyovyote iwavyo, futuhi hujikwepesha na masuala ya kutia hofu au kushtua.
Athari ya futuhi (kuchekesha) hutokana na matendo, mienendo ya wahusika na hitilafu au ila za kuingiliana kwa kiusemi. Futuhi huwa na viwango mbalimbali vya kuchekesha.
Kwanza, kuna kiwango hafifu (duni) ambacho huhusishwa na futuhi ya chini. Kuna baadhi ya kazi ambapo kiwango cha kuchekesha huwa kigumu kutambulikana na huhitaji utambuzi mpevu. Hii ni sifa ya aina ya futuhi iitwayo Futuhi ya Juu.
Aina zingine ni pamoja na, futuhi ya kikanivali, kitashtiti, maadili, mawazo, ucheshi na zimbwe. Mifano mizuri ya futuhi ni ‘ Aliyeonja Pepo’ (Topan, F.), ‘ Usaliti Mjini’ (Imbuga, F.),
Twelfth Night (Shakespeare, W.),
Importance of Being Earnest (Wilde Oscar), Mkaguzi Mkuu wa Serikali (Gogol, Nikolai), The Lion and the Jewel (Soyinka, W.) na ‘ Masaibu ya Ndugu Jero’ (Soyinka, W.).

MELODRAMA
Katika zama za urasimi, aina hii ilitumiwa kuelezea aina ya drama au tamthiliya iliyokuwa na matumizi mengi ya uimbaji au nyimbo (melos). Kwa hiyo, melodrama ni dhana inayotumiwa kuelezea aina ya tamthiliya ambayo imetawaliwa na uimbaji wa nyimbo.
Melodrama inafanana sana na tanzia ingawa mara nyingi nguli wa melodrama humalizika na ushindi, matokeo yake yanasisimua sana na mwendo wa msuko wake huwa ni wa haraka haraka zaidi. Wahusika wake huvutia na kufurahisha lakini hawana sifa za kishujaa.
Dhamira ya melodrama huzungukia mvutano kati ya wema na uovu au ubaya. Miishio ya tamthiliya hizi haina sifa ya mtakasohisia kama ilivyo na tanzia bali huwa ni aina ya ushindi wa mhusika mwema. Mfano mzuri ni ‘ The Begger’s Opera’ iliyotungwa na mwanatamthiliya wa Kiingereza John Gay kunako 1728.

TANZIA-RAMSA
Ni tamthiliya inayochanganya vipengele vya tanzia na ramsa, hutumiwa sawa na tamthiliya za kibwege - hii ni tamthiliya ambayoinaonyesha kwamba kicheko au furaha ndiyo jibu pekee la maisha kwa watu ambao hawana imani na maisha ambayo kwayo misingi thabiti ya maisha imeondolewa. Mfano tamthiliya ya Amezidi ya S.A Mohamedi
Tanzia-ramsa ni aina huonyesha mabadiliko ya aina fulani yanayogeuza mwelekeo wa matukio ya kitanzia na kuufanya kuwa tofauti au wa kufurahisha. Hali hii inaweza kupatikana kwa kuwepo kwa hasidi au mui anayetubu na kuyajutia makosa au msimamo wake au kuwepo kwa mandhari ya kiulimbwende.
Kimsingi, tanzia-ramsa ni tanzia inayoishia kwa furaha. Kinyume chake ni futuhi zimbwe. Dhana hii inaakisi kwa kiasi kikubwa baadhi ya mitazamo ya kidhanaishi ya fasihi ambapo ushujaa na tanzia havijitokezi katika hali ya kawaida kama vilivyozoeleka.
Hali hii inadhihirika katika tamthiliya kama vile ‘ The Cherry Orchard’ (Anton Chekhov, 1904), ‘ The Winter’s Tale’ (William Shakespeare, 1611).

FUTUHI/KOMEDIA (COMEDY)
Futuhi au komedia ni utungo ambao unachekesha na kuchangamsha. Tamthiliya ya aina hii inaweza kusawiria picha yakini katika maisha kwa undani ikitumia dhihaka na kejeli kwa kuchekesha. Futuhi huficha ukali wa masuto kadri inavyoendelea kuburudisha hadhira yake.
Futuhi hulenga kurekebisha tabia inazozidhihaki au inazozicheka. Kusema futuhi inafurahisha haina maana kuwa dhamira yake haina uzito. Futuhi huzungumzia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa njia ya kuchekesha. Futuhi huweza kuwa na sifa zinazotofautiana – jambo ambalo hutumiwa kama kigezo cha kuainisha aina mbalimbali. Lakini vyovyote iwavyo, futuhi hujikwepesha na masuala ya kutia hofu au kushtua.
Athari ya futuhi (kuchekesha) hutokana na matendo, mienendo ya wahusika na hitilafu au ila za kuingiliana kwa kiusemi. Futuhi huwa na viwango mbalimbali vya kuchekesha.
Kwanza, kuna kiwango hafifu (duni) ambacho huhusishwa na futuhi ya chini. Kuna baadhi ya kazi ambapo kiwango cha kuchekesha huwa kigumu kutambulikana na huhitaji utambuzi mpevu. Hii ni sifa ya aina ya futuhi iitwayo Futuhi ya Juu.
Aina zingine ni pamoja na, futuhi ya kikanivali, kitashtiti, maadili, mawazo, ucheshi na zimbwe. Mifano mizuri ya futuhi ni ‘ Aliyeonja Pepo’ (Topan, F.), ‘ Usaliti Mjini’ (Imbuga, F.),
Twelfth Night (Shakespeare, W.),
Importance of Being Earnest (Wilde Oscar), Mkaguzi Mkuu wa Serikali (Gogol, Nikolai), The Lion and the Jewel (Soyinka, W.) na ‘ Masaibu ya Ndugu Jero’ (Soyinka, W.).

MELODRAMA
Katika zama za urasimi, aina hii ilitumiwa kuelezea aina ya drama au tamthiliya iliyokuwa na matumizi mengi ya uimbaji au nyimbo (melos). Kwa hiyo, melodrama ni dhana inayotumiwa kuelezea aina ya tamthiliya ambayo imetawaliwa na uimbaji wa nyimbo.
Melodrama inafanana sana na tanzia ingawa mara nyingi nguli wa melodrama humalizika na ushindi, matokeo yake yanasisimua sana na mwendo wa msuko wake huwa ni wa haraka haraka zaidi. Wahusika wake huvutia na kufurahisha lakini hawana sifa za kishujaa.
Dhamira ya melodrama huzungukia mvutano kati ya wema na uovu au ubaya. Miishio ya tamthiliya hizi haina sifa ya mtakasohisia kama ilivyo na tanzia bali huwa ni aina ya ushindi wa mhusika mwema. Mfano mzuri ni ‘ The Begger’s Opera’ iliyotungwa na mwanatamthiliya wa Kiingereza John Gay kunako 1728.

2. RAMSA/KOMEDI
Ni tamthiliya ambayo inachangamsha na huishia kwa kufurahisha na ni ya vichekesho, hii haina maana kwamba haina maudhui mazito ndani yake.
Inashughulikia mambo yale yale yanayoweza kushughulikiwa na tanzia. Mfano masuala ya unafiki,uzembe, wivu, hivyo inayashughulikia kwa namna tofauti na tanzia
Udhati wa ramsa si kwamba usanii humalizika katika kicheko/furaha zaidi ni kuishia mhusika mkuu kufanikiwa
Shujaa wa kiramsa
· Si lazima awe mtu maalum/mbabe au shujaa, anaweza kuwa mtu wa kawaida
· Mhusika wa ramsa lazima awe mtu wa wastani chini ya wastani, awe ni mtu ambaye hatarajiwi kujitokeza na mtu wa nasaba duni na matendo yake yawe ya ucheshi
· Ni lazima awe mtu ambaye akifanikiwa wasomaji au watazamaji watafurahi
Uhusika katika ramsa
· Ramsa inawahusu watu wa kawaida kuliko ilivyo tanzia
· Inawahusu watu wa kipato cha kati na cha chini
· Dhamira zote huelekezwa kwa watu wa kipato cha chini na duni. Mfano walalahoi

SIFA ZA RAMSA
Sharti ivutie akili na siyo hisia
Ni lazima kuwa na matendo bila kufikiria hii itapelekea msomaji au mtazamaji kujua kwamba wahusika hawa hawana akili
Lazima iwe na hali ya utu (ikitukumbusha ubinadamu wetu)
Sharti iwe na mila na desturi ambazo hadhira inazifahamu toka katika jamii yake
Hadhira isiogope au kupata uchungu kwa sababu hii sio lengo lengo la ramsa
Wahusika wa ramsa hujaribu kuepuka vikwazo ambavyo vimewekwa
Inaonyesha haja ya kuikomboa nafsi Mfano wa ramsa ni kama vile Mfalme Juha.

MAREJELEO
Muhando,P. (1982), Lina Ubani, Dar es Salaam University Press: Dar es Salaam.
Wamitila, K.W. (2003), Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi . English press: Nairobi
Senkoro, F. E. M. K. (2006), Kioo cha Lugha, Fasihi ya Kiswahili ya Majaribio; Juzuu namba (4)
Director AY. Karibu tena na tena

Thursday, November 16, 2017

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI. AY director

Uhakiki wa Kazi za Fasihi

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
DHANA YA UHAKIKI

Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k
DHIMA YA UHAKIKI NA NAFASI YA MHAKIKI
Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo:
Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa urahisi
Watunzi wa kazi za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo mhakiki anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi kwa kuvifafanua kwa lugha rahisi.
Husaidia ukuaji wa kazi za fasihi
Mhakiki anapoonesha ubora na udhaifu wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na kutunga kazi iliyobora zaidi.
Uhakiki hukuza uelewa wa mhakiki
Kwa kuhakiki kazi mbalimbali za fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja na mambo yanayotokea katika jamii.
NAFASI YA MHAKIKI
Mhahiki ana nafasi kubwa katika kazi za fasihi, Mhakaki ndiye anafafanua kazi ya fasihi ili hadhira iweze kumwelewa vizuri mtunzi wa kazi hiyo. Kwa hiyo hapa mhakiki anasaidia kurahisisha mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi.
Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.
HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA UHAKIKI
Hatua anazopitia mhakiki ni pamoja na hizi zifuatazo:
Kwanza ni kuisoma kazi ya fasihi; hapa mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.
Pili ni kuainisha na kuchambua mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hiyo katika vipengele vya fani na maudhui.
Tatu ni kutoa tathimini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.
MAMBO YANAYOCHUNGUZWA WAKATI WA KUFANYA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
Maudhui
Maudhui katika fasihi hujumuisha mawazo na pengine mafunzo mabalimbali yaliyomsukuma mtunzi ama msanii hadi akatunga kazi fulani ya sanaa. Huwa msanii huyo amakesudia hadhira yake ya wasomaji, wasikilizaji au watazamaji wayapate mawazo au mafunzo hayo; kwa hiyo haya twaweza kuyaita lengo la msanii kwa hadhira yake. Mawazo na mafunzo haya hayazuki hivihivi tu, kwa hiyo wakati wa kuyachambua na kuyajadili ni lazima yahusishwe na hali halisi ya kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi zilizopo katika jamii, hali hizi ndizo zilimzaa, zilimlea na kumkuza msanii.
Wakati wa kuchambua kazi za kifasihi mhakiki ni lazima ajiulize amaswali yafuatayo:
1. Je, msanii anatueleza nini?
2. Je, msanii kamtungia mtu wa tabaka gani?
3. Anamtukuza nani?
4. Anambeza nani?
5. Msanii anataka tuchukue ahatua gani katika utatuzi wa matatizo ayashugulikiayo katika kazi yake?
6. Migogoro aichunguzayo msanii ina umuhimu gani katika maisha ya jamii? Mafunzo falsa na maadili yaibushwayo na uchambuzi wa migogoro hiyo yana nafasi gani katika maendeleo ya jamii?
Vipengele vinavyochambuliwa katika maudhui
1. Dhamira
Dhamira ni sehemu moja wapo tu ya maudui ya kazi ya fasihi; ni lengo au mawazo makuu yanayojitokeza sana katika kazi ya fasihi.
1. Migogoro
Katika kipengele cha migogoro, tunapata migogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, famila zao, matabaka yao na kadhalika. Na migogoro hii aghalabu hujikita katika mahusiano ya kijamii, migogoro yaweza kuwa ya:
1. Kiuchumi
2. Kiutamaduni
3. Kisiasa
4. Migogoro kati ya wazo na wazo, falsafa na falsafa na baina ya hali na hali.
5. Halikadhalika kuna migogoro ya kinafsiya, itokeayo katika nafsi za wahusika.
1. Falsafa
Falsafa ni jumla ya mawazo, mafunzo na lengo la msanii katika kazi ya fasihi. Kwa maana nyingine falsafa ni mchujo wa welekeo wa mawazo muhimu yajitokezayo kila mara katika kazi mbalimbali za msanii. Hii inamaanisha kuwa sio rahisi kung’amua falsafa ya msanii katika kazi yake moja tu.
1. Msimamo
Msimamo wa msanii kuhusu maswala mbalilmbaili ya kijamii hubainishwa na mawazo, mafunzo, lengo na falsafa. Msimamo ndio uwezao kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaotunga kazi za fasihi zilizo na kiini na chimbuko moja.
Fani
Fani katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii katika kazi yake. Mambo mabalimbali yanaweza kuunda ama kubomoa kazi ya kutegemeana na vile msanii kayatumia.
Mambo yanayochunguzwa katika fani wakati wa uhakiki wa kazi za fasihi ni pamoja na haya yafuatayo:
Wahusika
Wahusika ni watu au viumbe waliokusudiwa wawakilishe tabia za watu katika kazi za fasihi. Wahusika wa fasihi ni wa aina kuu tatu:
Wahusika wakuu; hawa ni wale wanaojitokeza kila mara katika kazi za fasihi tangu mwanzo hadi mwisho. Maudui ya kazi ya fasihi huwa yanamzungukia na hata kutolewa na mhusika mkuu zaidi ya wahusika wengine. Mara nyingi jambo hili limewafanya wahusika wakuu wawe midomo ya wasanii.
Wahusika wadogo ; hawa hujitokeza hapa na pale katika kazi ya fasihi ili kuukamilisha ulimwengu wa kazi hiyo. Wakati mwingine wahusika wadogo huweza kusaidia kujenga dhamira fulani katika kazi ya fasihi na wakati mwingine wahusika hao huweza kusaidia kukuza dhamira kuu ya kazi ya fasihi.
Wahusika bapa; ni wahusika ambao hawabadiliki, hatuwaoni wakipita hatua mbalimbali za mabadiliko katika maisha yao. Wanabaki kuwa walewale katika kazi yote ya fasihi.
Wakati wa kuchambua kipengele cha wahusika, maswali yafutayo hayana budi kutafutiwa majibu yake:
1. Je, wahusika wamechorwaje?
2. Je, wahusika hao wanahusianaje wao kwa wao?
3. Je, wanatimizaje lengo la maudhui ya kazi ya fasihi waliomo ndani yake?
4. Je, wanaaminika?
5. Je, mtunzi kawachagulia majina gani? Hapa baadhi ya majina yanaweza kuwa ni ya kiishara yajengayo falsafa au hata mtazamo wa msanii.
6. Je, wahusika wote wametumia lugha moja au hata unaweza kumtambua mhusika kutokana na lugha anayoisema? Hapa tunataka kuona ikiwa lugha waliyotumia wahusika inamtambulisha kila mmoja wao toka tarafani, kazi anayofanya, mazingira yaliyomlea na pia mahali pake katika jamii.
Lugha
Fasihi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama kuandikwa. Kipengela cha lugha ni muhimu sana katika fasihi kwani ndicho hutenganisha fasihi na sanaa nyinginezo.
Matumizi ya lugha katika fasihi yapo ya aina mbalimbali, kuna tamathaili za semi, misemo, nahau, methali, lahaja za wahusika, uchaguzi wa msamiati, miundo ya sentensi.
Tamathali za semi
Tamathali za semi ni maneno, nahau au sntensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo, na hata sauti katika maandishi ama kusema. Hizi wakati mwingine hutumiwa kwa njia ya kuipamba kazi ya fasihi na kuongeza utamu wa lugha. Baadhi ya tamathali za semi ni pamoja na hizi zifuatazo:
Tanakali za Sauti
Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.
Tashbiha
Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. mfano, Mwembamba kama sindano; Chichi na Aisha wanao uzuri sawa na wa malaika.
Tashihisi
Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Mfano, "Sungura aliposhindwa, akasema sizitaki hizi mbichi".
Takriri
Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Mfano, alikimbia, alikimbia, alikimbia hadi akashika nafasi ya kwanza
Ukinzani
Ukinzani ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana.
Sitiari
Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Mfano; Maisha ni mlima, juma ni mwamba.
Taswira
Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
Taashira
Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.
Mfano; Jembe – mkulima, Mvi – mzee
Majazi
Hii ni aina ya sitiari ambayo itajapo sehemu tu ya kitu hapo hapo sehemu hiyo huashiria na kuwakilisha kitu hicho. Mfano; roho – mtu (Ajali ile imepoteza roho tano)
Lakabu
Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.
Chuku
Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu, kutilia Chumvi.
Msisitizo bayana
Tamathali hii husisitiza maana ya sentensi kwa kutumia kinyume. Kwa mfano; alikuwa ni msichana mzuri, ukimwona kwa mbali huwezi kujua kama anakuja au anakwenda.
Tabaini
Hii ni tamathali ya semi ambayo kwayo maneno au mawazo yanayokinzana hutumiwa katika sentensi ili kuleta msisitizo wa wazo ama mawazo yatolewayo.
Mfano; Usimwamini mtu. Atakuchekea kwa meno meupe huku ndani anakuchukia kwa roho nyeusi. Punda afe, mzigo wa bwana ufike.
Tashititi
Hii ni tamathali ya semi ambayo kwayo swali linaulizwa huku jibu lake linafahamika waziwazi. Kwa mfano, ikiwa mtu kapoteana na rafiki yake kwa muda mrefu halafu ghafula wanakutana huweza kumuuliza, “Aisee, ni wewe?” ijapokuwa anajua kuwa ni yeye.
Mjalizo
Katika tamathali hii sentensi huwa ni mfuatano tu wa maneno yasiyo na viungo vyovyote.
Mfano; - Nilikaa, nikasubiri nikachoka
Nilipanda, nikapalilia, nikavuna.
Semi
Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:
Nahau – ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la kufikisha maana iliyotofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo. Nahau huwa na vitenzi.
Misemo – ni semi fupifupi ambazo hutumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalumu. Misemo haina vitenzi.
Mubalagha
Tamathali hii hutia chumvi kuhusu uwezo wa viumbe, na kuhusu tabia zao na kuhusu sifa zao kwa madhumu ni ya kuchekesha au kusisitiza.
Mfano; Dah, cheki yule demu, ana mlima wa kiuno, Alipoachwa na mpenzi wake alilia hadi machozi ya damu.
Uzungumzi Nafsiya
Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
Ritifaa
Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.
Kuchanganya Ndimi
Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. Mfano, "alisimama kwanza kwa muda, before he went aliniambia nisimwambie mtu yeyote yule, you know!"
Kuhamisha Ndimi
Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu. Mfano: Kazi hii ni ngumu sana, sitaweza kuifanya. People are trying to convince me to stay here but I think I can't, I must go!
Methali
Methali ni sehemu ya lugha ambayo inaweza kufananishwa na kiungo cha lugha na kitoweo cha lugha pia…hutumiwa kwa kuyatafakari na kuyapima maisha, kufunzia jumuiya na kututawalia jamii na mazingira ya binadamu. Methali hufunua falsafa ya jamii na hekima ya wale wanaoitumia katika mazungumzo yao.
Pale ambapo methali zimetumika katika kazi mbalimbali za fasihi mara nyingi zimejenga fani na maudhui ya kazi hiyo.
Misemo na Nahau
Mara kwa mara matumizi ya misemo na nahau katika kazi za fasihi hushabihiana sana na yale ya methali. Misemo hutumika wakati mwingine kutambulisha mazingria maalum au kuijulisha hadhira wakati unaohusika katika kazi ya fasihi inayoshughulikiwa. Jambo hili linatokana na sababu kuwa misemo huzuka/huibuka na kutoweka kufuatana na hali mbalimbali za kimazingira.
Nahau ni msemo uliojengwa kwa kutumia maneno ya kawaida lakini ambao huwa umesitiri maana tofauti na ile inayobebwa na maneno hayohayo katika matumizi ya kawaida.
Mfano:
1. Joyce kavaa miwani – Joyce amelewa.
2. Tofa ana mkono wa birika – Tofa ni mchoyo
UHAKIKI WA MASHAIRI
Maana: - Shairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato unaowasilisha mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na hufuata utaratibu fulani.
Aina za mashairi
Mashairi yapo ya aina mbili:
1. Mashairi huru
2. Mashairi ya arudhi
Mashairi ya arudhi
Haya ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa mashairi. Arudhi/kanuni hizi ni pamoja na:
1. Kugawika kwa shairi katika beti
2. Beti kuwa na idadi maalum ya mishororo.
3. Mishororo ya ubeti kugawika katika vipande
4. Mishororo kuwa na ulinganifu wa mizani
5. Shairi kuwa na urari wa vina
6. Shairi kuweza kuimbika / kuwa na mahadhi au mapigo.
7. Kuwepo kwa kipokeo katika shairi
8. Kuwa na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwala
9. hairi kuwa na utoshelezo wa beti / kujisimamia kimaana.
Mashairi huru
Pia hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiozingatia lazima ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu huweza kuwa:
1. Lugha ya muhtasari
2. Lugha yenye mahadhi
3. Lugha ya kisanii iliyo na mafumbo na taswira
4. Mara nyingine hugawika katika beti.
5. Mishororo kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)
SIFA ZA MASHAIRI
Mashairi huwa na sifa maalum zinazoyatambulisha kama kazi ya kishairi, yawe ya kimapokeo au kimapinduzi.
Sifa hizi ni kama vile:
1. Mashairi hutumia lugha ya mkato / muhtasari
2. Ni sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundi
3. Huwa na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi beti.
4. Hutumia lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na jazanda.
5. Mashairi huwa na sifa ya kuweza kuimbika hivyo shairi ni wimbo na wimbo ni shairi.
Dhima ya mashairi
1. Kupasha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvuto
2. Kuelimisha na kuzindua jamii.
3. Kuendeleza na kukuza kipawa cha utunzi.
4. Kuhifadhi msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi.
5. Kuburudisha hadhira na wasomaji.
6. Kuwasilisha hisia za ndani za mtu na mawazo
Uhakiki wa Mashairi
Uhakiki wa shairi ni kuvunjavunja shairi katika sehemu zake na kuzichunguza kwa makini ili kueleza ujumbe, dhamira, maudhui na hali ya vipengee vya shairi.
Uchambuzi wa mashairi huweza kufanywa kwa hatua.
Hatua za uhakiki
1. Soma shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumla.
2. Soma shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali na kuchunguza maana ya  kila mojawapo
3. Pitia maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu yanayotarajiwa.
4. Soma shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu maswali.
5. Toa majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririko.
Vipengee vya Uchambuzi Wa Mashairi
1. Anwani/kichwa cha shairi – Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au sentensi moja. Anwani ni kidokezo muhimu cha kinachozungumziwa katika shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa moja, fumbo, kinaya, kibwagizo au sehemu ya kibwagizo.
Ikiwa shairi halina anwani, basi lipewe anwani inayoafikiana na maudhui au dhamira kwa sentensi isiyozidi maneno 6.
1. Maudhui – Haya ni masuala makuu au mambo muhimu yanayohusu mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi.
Kwa mfano: malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k. Maudhui hung’amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa kilichomo katika shairi.
2. Dhamira / shabaha - Ni lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake. Dhamira ya mtunzi huwa ni ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi katika shairi.
Mfano: Baada ya kusoma shairi, unaweza kung’amua mtunzi alitaka kusisitiza kauli kuwa uongozi mbaya haufai, misitu ni uhai n.k. Dhamira hutokana na mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa yake.
3. Mbinu na tamathali za lugha - Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi zilizotumiwa na mshairi katika shairi. Mfano:
1. Mazda / ziada / zidi - kurefusha maneno. Mfano: enda kuwa
enenda .
2. Inksari / muhtasari - Ni kufupisha maneno. Mfano: aliyefika kuwa
alofika.
3. Utohozi – Mbinu ya kugeuza msamiati / maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika kana kwamba ni ya Kiswahili.
Karibu tena
AY director

Wednesday, November 8, 2017

MITAZAMO KUHUSU HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI

Mitazamo kuhusu lugha ya kiswahili

wataalamu hudai kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni huko Kongo ambayo baadaye iliitwa Zaire na sasa inaitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Dai hili linaimarishwa na wazo lingine linalodai kwamba katika vipindi kongwe vilivyopat kuwako, sehemu za Pwani ya Afrika mashariki hazikuwa zimekaliwa na watu. Kutokana na hali ya vita, uchungaji na biashara, inadaiwa kuwa Wabantu walitoka sehemu za Kongo walisambaa na kuja pwani ya Afrika mashariki kupitia Kigoma. Baadhi ya wabantu hawa walipitia sehemu za Uganda. Wakati wa kusambaa kwao, walieneza pia lugha zao ikiwemo hii ya Kiswahili.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba, madai ya kuwa asili ya Kiswahili ni Kongo hayana msingi kwani mpaka sasa wataalamu wanaodai hivi hawajaweza kueleza na kuthibitisha kisayansi ama Kihistoria juu ya lini hasa watu walianza kuishi pwani ya Afrika mashariki.
Kiswahili ni Ki-Pijini au ni Ki-Krioli
(i) Kiswahili ni Ki-Pijini
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa Kiswahili ni Ki-Pijini. Wataalamu hawa hudai kwamba Ki-Pijini ni lugha ambayo huzaliwa kutokana na kukutanika kwa makundi mawili (A) na (B) yanayotumia lugha mbili tofauti. Ili makundi haya yaweze kuwasiliana kunaundwa lugha ambayo kitabia ni tofauti na zile zinazozungumzwa na makundi yanayohusika. Lugha hii inaweza kuwa na msamiati mwingi kutoka lugha kati ya zil mbili, au inaweza kuwa na msamiati wenye uzito sawa. Lugha hiyo ndiyo inayoitwa Ki-Pijini. Mazingira yanayosababisha kuwepo Ki-Pijini ni kam vile biashara, utumwa, ukoloni, nk.
Kwa mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwa kilianza kama Ki-Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyeji wa pwani y Afrika Mashariki na wageni wa kutoka Mashariki ya Kati, hususan Waarabu. Aidha, husisitiza kuwa lugha ya Kiswahili haikuwepo kabla ya hapo.
(ii) Kiswahili ni Ki-Krioli
Wataalamu hawa wanadai kwamba watu wanaozungumza Ki- Pijini wanaweza kuishi pamoja kwa muda wa karne nyingi na kwa hiyo wakaweza kuzoeana na hata kufikia hatua ya kuoana. Wakioana watot wao huikuta lugha ya ki-Pijini ama lugha yao ya kwanza. Inapofikia hatua ya aina hii kwa watoto wanaozungumza lugha hiyo, wao husemekana sasa
wanazungumza lugha ya Ki-Krioli, lugha ambayo ni hatua ya juu ya Ki-Pijini, yaani Ki-Pijini kilichokomaa.
Nadharia hii hutumia kigezo cha msamia wa Kiswahili kuonesha uhusiano uliopo kati ya Kiswahili na Kiarabu. Wanadai kuwa, msamiati mwingi wa Kiswahili unatokana na Kiarabu. Hivyo huhitimisha kuwa hapana shaka Kiarabu kimehusika katika kuizalisha na kuikomaza lugha ya Kiswahili.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba hutumia kigezo cha msamiati tu bila kuzingatia vipengele vingine vya lugha kama vile matamshi, maumbo ya manen au muundo wa sentensi za Kiswahili. Aidha, wataalamu hawa hawakuhoji sual la kufanana kwa Kiswahili na lugha jirani katika hayo yaliyotajwa hapo juu na katik eneo la Kijografia ambamo Kiswahili na lugha hizo nyingine hujikuta zikizungumzwa. Vigezo hivi ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa Kiswahili SI Ki-Pijini wala SI Ki-Krioli, bali ni lugha kama zilivyo hizo lugha jirani.
Kiswahili ni Lugha ya Jamii ya Vizalia
Kundi la kwanza la wataalamu wa nadharia hii, Bishop Edward Steera, Bwana Taylor, Dkt. R. Reusch, (Katika Maganga, 1997)  hudai kwamba:
· Waarabu na Waajemi waliohamia pwani ya Afrika ya Mashariki waliwao wanawake wa ki-Afrika.
· Watoto wao walijifunza maneno y Kiarabu na ki-Ajemi kutoka kwa baba
· Aidha, watoto hao wakajifunza maneno ya ki-Bantu kutoka kwa mam zao.
· Katika jitihada zao, watoto hao walijirekebisha kutokana na tamadun wazazi wao ambazo ni tafauti: utama wa Kiarabu na utamaduni wa ki-Bant
· Vizalia hawa wakaanza kutumia lu mpya ya mseto wa Kiarabu, Kiajemi n lahaja mbalimbali za ki-Bantu.
· Kwa kiasi kikubwa, lugha mpya ya mseto ilikuwa ni upotoshaji wa lugha Kiarabu na Kiajemi.
· Mwarabu au Mu-Ajemi alikuwa muumini wa dini ya Uislamu.
· Umo humo, vizalia hawa wakayain maneno ya Kiarabu, Kishirazi na Kihin katika hii lugha mpya.
· Pamoja na kuyaingiza maneno ya kigeni, lugha-mpya yao hii (Kiswahili), ilikithiri vionjo vingi vya lugha mbali za ki-Bantu.
· Ndipo baadaye, lughampya yao hii ikajulikana au kuitwa Kiswahili.
· Kwa maoni ya wataalamu hawa, sehemu mbili kati ya tano (2/5) ya maneno yanayotumika katika lugha hi mpya ni ya ki-Bantu.
· Sarufi ya lugha mpya hii ni mseto ki-Bantu (chenye utata na kisicho na mpangilio maalumu) pamoja na Kiara (chenye mantiki na kilichokomaa).
Kundi la pili la wataalamu wa nadharia hi B. Krumm na F. Johnson lina mawazo yanayodai kwamba:
· Kiswahili kilitokana na visiwa vya Lamu, Kilamu/Kiamu.
· Wageni kutoka Ghuba ya Ushirazi/Uajemi na Arabia ya Kusini walikuja k Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha tofauti.
· Lakini kutokana na kuoana kwao wenyeji, wageni hawa wakaichukua lu ya hapo walipofikia, wakaikuza kwa maneno kadhaa na sentensi kadhaa kutoka lugha zao za asili, yaani Kiara Kiajemi na Kihindi hususan katika masuala ya  biashara, ubaharia, vyom vya kazi zao na nguo.
· Aidha, utumwa na tabia ya kuoa wengi ilisaidia kutoa kundi kubwa la masuria. Hali hii ikaondosha hisia za ugeni katika lugha zao; na maneno y yakabatizwa kuwa ya ki-Bantu, na hat kupoteza kabisa sura ya ugeni.
Kiswahili ni Kiarabu
Kuna hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumia kutetea nadharia hii kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.
(i) Inadaiwa kuwa maneno yenye a Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni tosha kwamba lugha hii ilianza kam Pijini ya Kiarabu.
(ii) Inahusu neno lenyewe Kiswahili asili yake ni Kiarabu. Neno Kiswahili linatokana na neno “sahili” (umoja) “swahil” (wingi) lina maana ya pwan
(iii) Inadaiwa kwamba kwa kuwa Kisw kilianza pwani, kwa kuwa idadi kub sana ya wenyeji wa pwani ni waisla kwa kuwa uisilamu uliletwa na Waar basi Kiswahili nacho kililetwa na W
Kiswahili si Kiarabu
Madai kwamba Kiswahili si Kiarabu yanathibitishwa na hoja kinzani zifuatazo
Tukianza na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya Kiarabu’ tunaona wazi kwamba madai haya hayan mashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa na maneno ya mkopo yenye asili ya Kiarabu (na kwa hakika yapo yenye asili y Kiajemi, Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyeji wa pwan na wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbili tofauti wanapokutana hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lugha kuwa na maneno mengi ya mkopo kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyo isemekane kuwa imetokana na hiyo lugha nyingine.
Pili wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe Kiswahili lina maana ya Kiarabu.
Kwani linatokana na neno “sahili” (umoja na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewe jina lake, yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine: Jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. Na hivi ndivyo ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaani Waswahili,
walipotembelewa na Waarabu na kuitwa As-Sahilyy au As-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake Sawahil), yaani pwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko !
Kigezo cha dini nacho hakikubaliki lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya Kiarabu yenyewe ilikuwep karne nyingi kabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu. Hali kadhalika, lugha nyingine z Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabl ya kufunuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani s ukristo, basi ndivyo vivi hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini ya uislamu, aslan! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachoweza kufanya ni kuitumia lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dini kuifasili lugha.
Kiswahili ni Kibantu
Vipengele vinavyotumika katika kuihalalisha nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kibantu ni ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa ki-Historia na kuichunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyik wa kusambaa kwa lugha za ki-Bantu. Wataalamu wa nadharia hii wanahitimish kwa kudai kwamba Kiswahili ni mojawap kati ya lugha katika jamii kubwa ya lugha za ki-Bantu.
Baadhi ya wataalamu muhimu wanaoiunga mkono nadharia hii ni Prof. Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl na Prof. Clement Maganga.
Profesa Malcom Guthrie ni mtaalamu (mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliwa na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana kama Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000 kutoka lugha 20 za Kibantu. Katika uchunguzi wake alikut mizizi (mashina) 2,300 imezagaa
katika lugha mbalimbali za Kibantu na Kiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi 500
yalilingana katika lugha zote 200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu. Mashina haya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongo kwa asilimia arubaini na nne (44%).
Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina hayo 500 yaliyomo katika kila lugha, mgawo uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:
Kiwemba kizungumzwacho Zambia -
54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga -
51%
**Kikongo kizungumzwacho Zaire           -
44%**
**Kiswahili kizungumzwacho Afrika Mashariki 44%**
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania 41%
Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji - 35%
Sotho kizungumzwacho Botswana - 20%
*Kirundi kizungumzwacho Burundi -
43%*
Kinyoro kizungumzwacho Uganda -
37%
Kizulu kizungumzwacho Afrika Kusini -
29%
Baada ya kupata matokeo haya, Profesa Malcom Guthrie anaiunga mkono nadharia hii ya kwamba Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudai kwamba:
(i) Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio w wageni;
(ii) Anaonyesha kwamba Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za Kiba
(iii) Mwisho anasema Kiswahili kilianzia ya Afrika Mashariki.
Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl: Wataalamu hawa wanaamini kwamba:
(i) Wakati wa utawala wa Shir katika upwa wa mashariki ya Afrik kulikuwa na kabila la Waswahili;
(ii) Kabila hili ni dhuria ya Wazar leo.
(iii) Kwa kuwa hawa Wazaramo w wamezaliwa katika harakati za kib kwa hivyo wakafuata nyayo za wa wao.
(iv) Lugha yao ilikuwa ya aina ya
(v) Kwa kuwa Wabantu ni wengi kuliko jamii ya makabila mengine, yao ya Kiswahili ikaanza kutumika kuenea katika makabila mengine, katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki.
(vi) Baadaye, Waswahili hawa ha wakafanya biashara na wageni wa kuvinjari Afrika Mashariki, hususa Waarabu, Washirazi, Wamalaysia, na Wareno ambao tayari walikuw wamefurika katika pwani hii ya Afr Mashariki miaka kadhaa kabla.
(vii) Vifaa na majina ya vitu vya bia vya wageni hao vikaselelea na kui katika mfumo wa lugha hiyo ya W ambayo ni ki-Bantu.
Madai ya nadharia hii yakichunguzwa, tunagundua kwamba inazingatia mitazamo miwili yaani, mtazamo wa ki-Isimu na mtazamo wa ki-Historia. Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea kukubalika na wataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu asili au historia ya Kiswahili.
Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwamba Kiswahili ni ki-Bantu. Kama tulivyoona, lugha ya Kiswahili ilifanyiwa utafiti na uchambuzi na wanataaluma kadhaa kwa madhumuni ya kuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bantu a la. Prof. Maganga alifanya uchambuzi wa ki-Isimu na wa ki-Historia kuhusu lugha hii. Matokeo ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha ya Kiswhili (au lugha kwa ujumla) unadhihirisha mambo mengi, mojawapo ni asili ya lugha hiyo. Amethibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha kw ushahidi thabiti hoja ya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl kama tulivyoieleza hapo juu.
(i)        Ushahidi wa Kiisimu
(a) Msamiati
Matokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.
Mfano:
Kiswahili Kindali Kizigua   Kijita
Kikurya Kindendeule
Mtu Umundu Mntu
Omun Omontu Mundu
Maji Amashi Manzi
Amanji Amanche Maache
Moto        Umulilo Moto
Omulilo Omoro Mwoto
(b) Tungo (Sentesi) za Kiswahili
Miundo ya tungo (sentesi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana na miundo ya tungo za maneno ya ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zina kiima na kiarifu.
Mfano:
Lugha za Kibantu
Kiima kiarifu
Kiswahili
Juma                           anakula ugali.
Kizigua
Juma                           adya ugali.
Kisukuma
Juma                           alelya bugali
Kindali
Juma                           akulya
ubbugali.
Kijita
Juma                           kalya ubusima.
Kindendeule
Juma                           ilye ughale.
(c)      Ngeli za Majina
Wanataalamu wanakubaliana kuhusu nge za majina kwa mujibu wa:
maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja; na
upatanisho wa kisarufi katika sentesi.
Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki hufuata maumbo ya umoja na uwingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja n uwingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana maumbo dhahiri ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu
Umoja Wingi
Kiswahili mtu
watu
mtoto
- watoto
Kikurya omanto
- banto (abanto)
omona - bana
(abana)
Kizigua mntu
bhantu
mwana
- bhana
Kindali                                   mundu
- bhandu
mwana
- bhana
Kindendeule mundu
βhandu
mwana
- βhana
Kigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi: Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi) na vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu. Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu Umoja -
Wingi
Kiswahili Baba analima
Baba wanalima
Kindali Utata akulima
Abbatata bbakulima
Kikurya Tata ararema
Batata(Tata)bararema
Kijita Tata kalima                        - Batat abalima
Kindendeule Tate ilima
Akatate βhilima
(d) Vitenzi vya Kiswahili na Kibantu
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo:
Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za ki-Bantu hujengw na mzizi (kiini) pamoja na viambishi vyak vya awali na vya tamati.
Mfano:
Kiswahili - analima          =
a – na – lim - a
Kiikuyu - arerema =
a – re –  rem–a
Kindali - akulima =
a - ku – lim – a
1 - 2 - 3 - 4
Sherehe:
1   -     Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.
2   -     Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo).
3   -     Mzizi/Kiini.
4   -     Kiambishi tamati.
Mnyambuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko w vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha za ki-Bantu.
Mfano:
Kiswahili - kucheka -
kuchekesha -           kuchekelea.
Kindali - kuseka -
kusekasha - kusekelela.
Kibena - kuheka           -
kuhekesha -           kuhekelea.
Kinyamwezi - kuseka -
kusekasha - kusekelela.
Kikagulu - kuseka -
kusekesha - kusekelela
Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi  vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za ki-Bantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, kama ifuatavyo:
Mfano:
Kiswahili - N i-nakwenda
Kihaya - Ni-ngenda
Kiyao - N- gwenda
Kindendeule - Ni- yenda
Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu na Kiswahili huishia na irabu –a.
Mfano:
Kiswahili kukimbi-a - kuwinda - kushuk-a
Kindali kukind-a -
kubhing-a - kukol-a
Kisukuma kupil-a -
kuhwim-a - Kutend-a
Kisunza kwihuk-a -           kuhig-a - kising-a
Kindendeule kuβhutuk-a -
kuhwim-a - kuhuk-a
tafiti wa Prof. Maganga kuhusu ushahidi wa ki-Isimu wa kuthibitisha kama Kiswahili ni ki-Bantu au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwa mifano mingine ifuatayo:
Mfano wa 1:
Lugha Se
Kiswahili
Kipare
Kindamba
Kichaga
Kihaya
Kikaguru
Kindendeule
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
anafuga
erisha
kafugha
nao he
n’afuga
kachima
ifuga
mbuz
mbuji
mene
mbur
embu
m’eh
mbuh
Katika mfano huu inaonekana kwamba mpangilio wa maneno katika sentesi una ufanano kwa sababu katika kila sentesi kuna kiima na kiarifu. Katika kiima kuna nomino, yaani jina la mtenda (Jongo) na katika kiarifu kuna kitendo kinachofanyik na nomino mtendwa. Pia nafasi ya viunganishi ni ile ile kwa lugha zote zilizoonyeshwa katika mfano huu.
Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio huu.
Mfano wa 2:
Lugha Sente
Kiswahili
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kizigua
Sitamkuta kesho
Timushangemu n
Natusanga inton
Tumuhanga fady
Nesikemkiche ya
Sirambila luvi
Katika sentensi hizo mpangilio wa maneno una ufanano kwa sababu kila sentensi ina kiima na kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Pia kiambishi cha nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza mwanzoni mwa neno la kwanza la kila sentesi.
Si tamkuta; Ti mushangemu;
Natusanga;
Tu muhanga;
Nesikamkiche; Si tambila.
Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia vinaonyesha hali ya ukanushi katka kila sentesi na nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.
Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika kitenzi cha kila sentesi.
Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sita m kuta,
timushangemu, na tu sanga, tumuhanga, nesika m kiche, na sita m bwila ni vya urejeshi; vinawakilisha nomino mtendwa.
Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo ya sentensi hizi inafanana na vitenzi vyake vina tabia mbalimbali, kam vile:
(i)        kubeba viambishi vya nafsi, mtenda na mtendwa,
(ii)       kuonyeshga hali ya ukanushi njeo za wakati na kitendo kinachofanyika.
Mfano wa 3:
Lugha
Kiswahili
Kizigua
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kindendeule
Akija
Akez
Kalaij
Ulu n
Newa
Ekiza
Anda ango
Katika sentesi hizo inaonekana kwamba sentesi zote zinafanana kimpangilio. Pia maneno yake yanakubali uambishaji, kwa mfano:
(i)        Katika maneno ya mwanzo:
akija, akeza. kalaija, akuja, newaj herufi zilizopigiwa vistari ni viamb nafsi vinawakilisha dhana ya mten
(ii)       Vivyo hivyo katika maneno:
anifuate, ampondele, anitimile, an aniratere, angobhekeraye, viambis vilivyoko katika viarifu vya sentesi vinawakilisha nafsi za watenda.
(iii) Pia vitenzi vya sentesi hizo vina ta kubeba virejeshi vya nafsi kama ili katika, m wa m bie, omu gambile, na ha li, m b we le na u m ti, vinaonye na hali ya uyakinifu- hali inayoony ufanano wa maumbo ya maneno.
(iv)      Licha ya kuwa na mpangilio unaof na wa lugha nyingine za kibantu, k mfano, katika mifano tuliyoiona h baadhi ya maneno yanafanana: ta maneno:
kafugha (Kindamba); nafuga
(Kihaya);
nifuga (Kindendeule); anafuga
(Kiswahili).
Pia maneno:
nkuku  (Kipare); nguku (Kindamba);
nguku (Kichaga); enkoko
(Kihaya);
ng’uku (Kikaguru);
nguku(Kindendeule);
nguku (Kindendeule)
Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana ufanano:
Akeza (Kizigua); kalaija
(Kihaya); alize (Kisukuma),
newaja  (Kinyaturu); ekiza
(Kipare); anda ahikite,... (Kindendeule);
akija, (Kiswahili.)
Pia maneno;
umugambe (Kizigua); omugambile
(Kihaya); unongeraye (Kindendeule);
na mwambie (Kiswahili).
Ufanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno pamoja na wa mpangilio wa maneno katika sentesi, vyote vinathibistisha kwamba lugha ya Kiswahil ni ya kibantu kama zilivyo nyingi nyinginezo.
(ii) Ushahidi wa Kihistoria Kwamba Kiswahili ni Kibantu
Baada ya kuangalia ushahidi wa kiisimu kuhusu asili ya Kiswahili, katika sehemu hii Maganga (1997) aliendelea kuchambu ushahidi wa Kihistoria unaothibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa katika upwa wa Afrika Mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kama vile Waarabu na Wazungu. Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika hapa Afrika Mashariki. Wote wanathibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa hapa Afrika Mashariki kabl ya ujio wa wageni.
(a) Ugunduzi wa Ali-Idris (1100-1166)
Ugunduzi huu yasemekana ulifanywa huk Sicily yapata mwaka 1100-1166. Kwenye mahakama ya mfalme Roger II. Licha ya kufahamika kuwa Kiswahili, kilipata kuandikwa kabla ya 10BK. Ali-Idris alikuwa wa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa ni Unguja. Katik maelezo yake anaandika pia majina kam vile kikombe, mkono wa tembo, muriani, na kisukari, ambayo ni ya ndizi mbalimba zilizokuwa zikipatikana huko.
(b) Ushahidi wa Marco Polo
Huyu ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na masuala mbalimbali ya kijiografi na alisafiri sehemu nyingi duniani. Marco Polo aliandika hivi:
“Zanzibari ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wa maili 200. Wat wote wanaabudu (Mungu), wana Mfalme na wanatumia lugha yao, na hawalipi kod (ushuru) kwa mtu.” Safari za Marco Polo 1958:301
Marco Polo anasemekana aliandika pia kitabu cha jiografia ambacho hakikupata kuchapishwa lakini sehemu zake zimepata kufasiriwa kwa Kirusi na Kifaransa. Mfano mmojawapo ni huu unaofuata:
“Katika visiwa vya Sjawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii, ni kile kisiwa cha Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao. Zanguabar/Ungudya, na wakazi wake, japokuwa ni mchanganyiko, kwa sasa wengi wao ni Waislam…chakula chao kikuu kikiwa ndizi. Kuna aina tano ambaz zinajulikana kama kundi, fili, ambazo uzito wake waweza kuwa wakia 12, Omani, Marijani, Sukari....”
Maelezo haya ya Marco Polo yanathibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha yao; mintarafu ya dini, chakula na utamaduni wao kwa ujumla.
(c) Ushahidi wa Al-Masudi (915 BK)
Katika moja ya maandiko yake, Al-Masud anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina l “wazanji”. Kwa dhana hii, neno Zanzibar linatokana na Zenzibar yaani “Pwani ya Zenji”. Katika maelezo yake Al-Masudi anaonyesha kwamba Wazenji walikuwa
“Watawala Wakilimi” ambao waliaminiwa kuwa walitawala kwa nguvu za Mungu. Kuna maelezo kuwa huenda neno “wakilimi” lina maana ya “wafalme”. Al-Masudi alisisitiza katika maelezo yake kuwa Wazenji walisema lugha kwa ufasaha na walikuwa na viongozi waliowahutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno “zenji” kuna uwezekano kuwa kabla ya majilio ya Waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au “Kizanji” na wageni waliofika pwani.
(d) Ushahidi wa Ki- Historia wa Mji wa Kilwa
Kimsingi habari zinazoeleza historia ya mji wa Kilwa katika karne ya 10-16BK zinataja majina ya utani kama vile:
mkoma watu, nguo nyingi, nk. ambayo walipewa Masultani wa kwanza wa Kilwa Ali Ibn Hussein na mwanae Mohamedi Ib Ali. Kutokana na habari hizi huenda lugh ya Kiswahili ilishaanza kusemwa mnamo karne ya 10 au ya 11 BK. Maelezo ya kihistoria yanaeleza juu ya Sultani aliyeitwa Talt Ibin Al Husaini ambaye alipewa jina la utani “ Hasha Hazifiki”.
(e)      Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK) kama Ushahidi
Shairi la zamani kabisa lililopata kuandikwa la Kiswahili, linalojulikana ni lile la Utenzi wa Fumo Liyongo . Utenzi hu inasemekana uliandikwa karne ya 13BK. Kuweko kwa shairi hili kunadhihirisha kuwako kwa lugha ya Kiswahili kabla ya karne hiyo, na kwa hivyo, huenda Kiswahili kilianza kutumika kabla ya karn ya 10BK. Baadhi ya beti za utenzi wa Fumo Liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti 6: Liyongo Kitamkali,
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na hiba huongeya.
Ubeti 7: Kilimo kama mtukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu huja kwangaliya.
Ubeti 10: Sultani pate Bwana
Papo nae akanena
Wagala mumemwona
Liyongo kiwatokeya.
(Kutoka E.A. Swahili Committee 1973)
Lugha hii ndio mfano wa lugha iliyokuwa ikitumika kunako karne ya 13BK. Ni wazi kuwa lugha hiyo ilianza kusemwa mapema kabla ya muda huo. Hoja za kihistoria inaelezea historia ya lugha ya Kiswahili toka karne ya 10BK hadi karne ya 18BK. Kutokana na ushahidi huu ni dhahiri kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Wabantu wa Afrika ya Mashariki.
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu

Asante kutembelea blog yangu, karbu tena.
AY director

CHIMBUKO LA KISWAHILI

Chimbuko la kiswahili

Bismillahi (tamko la kuashiria kuanza jambo jema kwa jina la Mwenyezi Mungu)! Yafuatayo ni maelezo ya Kamusi la Kiswahili Fasaha, chapisho la Baraza la Kiswahili la Zanzibar, mwaka 2010.
“Kiswahili, kama zilivyo lugha zote duniani kilianza kusemwa na kundi la watu waliojinasibu kwa sifa za kijamii zilizowaunganisha na kisha kusambaa katika makabila mbalimbali ya mwambao wa Afrika Mashariki, kuanzia Barawa hadi Sofala pamoja na visiwa vilivyo karibu na mwambao huo.
“Kumekuwa na hali ya kutafautiana miongoni mwa wataalamu juu ya chimbuko la Kiswahili. Nadharia kadhaa zimetolewa katika kujaribu kubainisha asili ya lugha ya Kiswahili.

1.“Nadharia mojawapo ni ile inayotoa hoja kuthibitisha kuwa Kiswahili ni Krioli (lugha ya awaliya wazungumzaji iliyoibuka kutokana na mchanganyiko wa lugha nyingi) iliyoibuka kutokana na mwingiliano wa lugha fulani za Kibantu na Kiarabu.

2.“Nadharia nyingine ni ile inayodai kuwa Kiswahili ni Kiarabu.

3.Nadharia ya tatu inatoa hoja kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kibantu.
“Nadharia hii ya tatu imekubalika miongoni mwa wataalamu kwa vile hoja zake zimethibitishwa kitaalamu kwa kutumia misingi ya isimu*”
*Isimu ni tawi la taaluma inayochunguza na kuchambua mifumo na miundo ya lugha, sayansi ya lugha. Ni mtaala ambao huchunguza lugha kama mfumo wa mawasiliano ya wanadamu. Huandama mikabala mbalimbali na tofautitofauti ya kisayansi na hivyo huwa na usayansi ndani yake.
(i) Utoshelevu wa kiutenzi: Isimu hudhihirisha uteuzi wa kiunzi fulani (kimoja maalumu) cha kiuchunguzi na wala si kingine.
(ii) Utoshelevu wa kiuchunguzi: Mwanaisimu hueleza yote yanayoonekana katika kongoo (mkusanyiko wa matini tofautitofauti zenye madhumuni maalumu ya kiutafiti) lililochaguliwa bila ya upungufu au mapuuza.
(iii) Utoshelevu wa kiufafanuzi: Isimu hushadidia (kitendo cha kutaka jambo lifanywe kwa hali yoyote) ufafanuzi wa viwango vyote: fonetiki, fonolojia, mofolojia, pragmatiki, semantiki na sintaksia.
(iv) Uchechefu (uchache, udogo): Tofauti zote za kongoo na lugha husika huwekwa dhahiri.
(v) Uwazi: Mawanda (eneo ambalo akili ya mtu yaweza kuwa na ufahamu nalo) ya sheria zinazohusika katika ufafanuzi wa lugha yapaswa kuwa wazi na yasiwe na utata wala kupingana.
Matawi ya Isimu: Isimu historia, isimu fafanuzi, isimu linganishi, isimu jamii, isimu tumizi, isimu Kiafrika, isimu falsafa, isimu tiba, isimu nafsia na isimu kompyuta. (Kamusi ya Karne ya 21 ukurasa
Kama kawaida naendelea kukukaribisha utembelee blog yangu Mara kwa Mara ili kupata mambo mengine mengi na mazur zaidi kisanue na kwa mshikaji apate kujua. Sayansinaafya.blogspot.com.
AY director

Monday, November 6, 2017

MITAALA TET:05206 classical NOTES Director AY official



          MITAALA

Maana ya mitaala. Ni jumla ya mipango na uzoefu ulioratibiwa kwa ajili ya mafunzo ya aina Fulani yanye malengo maalumu kwa wanafunzi. Mipango hiyo inaweza kuwa ni mambo ,matendo na uzoefu wa aina yoyote ile ambayo wanafunzi wanapata chini ya uongozi na usimamizi wa shule
Mawazo ya watalaamu
Ni jumla ya mipango na uzoefu ulioratibiwa kwa ajili ya mafunzo ya aina fulani.
WEMU: Mpango ulioandaliwa na kuratibiwa kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia.
TET (1994), Ukuzaji mitaala na Kunasihi: Ni jumla ya mambo yote yanayomwezesha mwanafunzi kupata uzoefu akiwa darasani au nje ya darasa.
Watunga mitaala: kuongozwa na malengo makuu ya Elimu kitaifa.
Hutugemea falsafa ya nchi.
Hutokana na siasa inayoongaza
Mfano:
Tanzania Falsafa ya Nchi: Ujamaa na Kujitegemea (Inatokana na siasa iliyokuwa ikiongoza ) Mwl J.K. Nyerere
Falsafa ya Elimu: Elimu ya Kujitegemea (Inatokana na falsafa ya Nchi)
Madhumuni/ Malengo Makuu ya Elimu Tz ( 9 yameanishwa katika Sera ya Elimu ya Taifa 1995)
Madhumuni/ Malengo ya Elimu kwa kila ngazi(Awali,Msingi,Sekondari na Elimu ya Juu)
Yameainishwa katika mihtasari ya masomo
Bila mwongozo wa falsafa ya nchi+ madhumuni ya Elimu kitaifa wakuza mitaala watakosa mwelekeo maalumu wa ukuzaji mitaala. Hivyo ina hitari ya kufanya mtaala uwe mkusanyiko wa mambo yasiyokuwa na mwelekeo maalumu kitaifa. Madhara yake ni watumiaji kkukosa mwelekeo na msimamo maalumu unaolingana na mwelekeo wa kitaifa.
SIFA YA MTAALA
• Kwa kawaida mtaala huzingatia taaluma (maarifa)ufundishaji (matendo ) na kujifunza (uzoefu) katika kiwango au ngazi Fulani ya elimu.
• Pia mtaala lazima uonyeshe walengwa wa mtaala (aina ya wanafunzi watakao tumia mtaala huo )kwa mfano chekechea ,watoto wa shule za msingi na sekondari na walemavu
• Muda utakaotumika kufundisha mtaala huo kwa mfano miaka miwili saba na minne mitatu mitano n.k)
• Sifa za walimu watakao fundisha mtaala huo mfano walimu wenye daraja A stashahada na shahada.
• Vifaa vitakavyotumika kufundishia walengwa na njia na mbinu zitakazo tumika kupima maendeleo ya wanafunzi na ubora wa mtaala.
• Steven George.
Kwa hiyo mtaala ni jumla ya mpango uliondaliwa kwa ajili ya kufundishia na kujifunza kwa lengo la kuwapatia walegwa maarifa ,stadi na mielekeo mbalimbali.
Nguzo kuu ya mtaala ni muhtasari ambayo hutumika katika kutekeleza mtaala huo.
Muhtasari –Ni mkusanyiko wa mada zinazokusudiwa ili kukamilisha kiwango fulani cha elimu , kazi au mafunzo maalumu.Katika shughuri za wakuza ukuzaji mitaala, wakuza mitaala wanapaswa kuongozwa na malengo makuu ya elimu yanayowekwa kitaifa.
UMUHIMU WA KUWA NA MTAALA
• Kudhibiti mfumo wa elimu
• Kuwaongoza walimu katika ufundishaji ili wasitoke nje ya malengo makuu ya elimu na falsafa ya nchi.
• Kuwezesha kurekebisha na kuendeleza elimu
• Kuweka malengo muhimu yaliyo kusudiwakufikia katika ufundishaji
• Mitaala ni dira na mwongozo muhimu kwa walimu katika ufundishaji
• Hutaja na uelekeza vifaa na nyenzo za kufundishia.
• Hulekeza malengo makuu ya elimu katika jamii husika.
• Huchukua taswira yote ya falsafa ya elimu ya nchi inayohusika.
MATUMIZI YA MTAALA
• Kusaidia walimu na wanafunzi kutambua malengo makuu yanayo kusudiwa kufikiwa katika utoaji wa elimu
• Kumfahamisha mwalimu na mwanafunzi kuhusu masomo au mada atakazo fundishwa ili kufikia malengo aliyojiwekea
• Kusaidia mwalimu kutambua na kuchagua njia za kufundishia zinazofaa ili aweze kufikia malengo aliyojiwekea.
• Kumsaidia mwalimu na mwanafunzi kuchagua na kufaragua vifaa vya kufundishia na kujifunzia mada mbalimbali.
• Kumwelekeza mwalimu kuhusu njia atakazo kupima maendeleo ya wanafunzi na ubora wa mtaala wenyewe.
AINA ZA MITAALA
1. Mtaala rasmi
2. Mtaala usiyo rasmi
3. Mtaala ficho
Mtaala rasmi
Ni mkusanyiko wa mambo yote anayopaswa kuyafanya na kuyafahamu mwanafunzi anapokuwa darasani.
Au ni mtaala uliopangwa kwa madhumuni ya kumfundisha mwanafunzi katika mfumo rasmi wa elimu.
SIFA ZA MTAALA RASMI
• Huanisha na kuweka wazi mambo ,matendo na uzoefu wa aina yoyote ile ambayo mwanafunzi ataupata chini ya uongozi na usimamizi wa shule yaani taaluma ufundishaji na kujifunza katika kiwango fulani cha elimu.
Huweka wazi aina ya walengwa
• Huweka wazi malengo ya kufundisha mtaala
AY director.
• Huweka wazi mambo , matendo na uzoefu ambao mwanafunzi ataupata chini ya uongozi wa shule au chuo.
• Huweka bayana njia ambazo mwalimu atatumia kufundishia
• Huweka bayana njia za kupima maendeleo ya mwanafunzi
• Huonyesha vifaa vitakavyo tumika kufundishia mtaala
• Huwa na muda maaalumu wa kutekelezwa
FAIDA ZA MTAALA RASMI
• Kupunguza tofauti zinazoweza kutokea iwapo kila shule au jamii itajitungia mtaala wake.
• Kurahisisha kuandaa vifaa vya kujifunzia
• Kurahisisha ufuatiliaji na upimaji wa maendeleo ya wanafunzi
• Huweka bayana utaratibu wa kutahini na sifa za wale watakaofuzu baada ya kufundishwa na kutahiniwa kwa kuutumia mtaala husika.
MAPUNGUFU YA MTAALA RASMI
Humfanya mwanafunzi ashindwe kufanya mambo yote yaliyo nje ya darasa kama vile ufugaji uvuvi, mila na desturi ya jamii yake.
MITAALA ISIYO RASMI
Ni mtaala unaofundisha mambo yote anayopaswa kujifunza mtoto nje ya mtaala ulio rasmi katika maisha ya kawaida ya kujifunzia . mara nyingine mtaala huu huitwa mtaala uliofichika.
Mara nyingi mitaala hiyo huandaliwa kulingana na mahitaji ya jamii ya mwanaafunzi na jamii husika kwa wakati ule.
SIFA ZA MTAALA USIO RASMI
• Hutokana na jamii au mazingira anayoishi mwanafunzi .
• Mada au mambo anayofundishwa zinalenga kumpatia mwanafunzi maarifa na stadi za kutatua matatizo aliyo nayo kwa wakari ule.
• Hukazia maarifa na stadi zinazo lenga kutatua matatizo yanayokabili jamii husika.
• Unaweza ukakoma mara matatizo yanapomalizika.
• Kwa kawaida haupangwi na kuratibiwa na njia kwa njia zilizo rasmi
• Mwanafunzi anaweza kupata maarifa na stadi bila kuwa chini ya usimamizi wa shule au chuo
• Mapungufu
Mwanafunzi hukosa ujuzi wa maarifa yaani mambo yote yanayofundishwa darasani katika mtaaala rasmi.
MAPUNGUFU
Mwanafunzi hukosa ujuzi wa maarifa, yaani mambo yote yanayofundishwa darasani katika mtaala rasmi.
MTAALA FICHO
Mtaala huu unajumuisha matendo yote yanayosaidia ujifunzaji usiokusudiwa au usioratibiwa. Kwa mfano ujifunzaji wa utii kwa mamlaka, kuwahi/kujali muda, usafiri nakadhalika. Yaani unajumuisha mambo yote ambayo hayaonekani kwenye muhtasari wa shule kama sehemu ya mtaala.
VIPENGELE VYA MITAALA
• Katika mtaala vipengele vilivyo muhimu ni vitano ambavyo hufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kutegemeana.
Steven George.
• Malengo ya mtaala
• Maudhui
• Njia za kufundishia
• Zana
• tathmini
Vipengele hivi vitano hufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kutegemeana kama viungo vya mwili wa binadamu. Ni vigumu kuvitenganisha ila kwa faida ya kujifunza na kuelewa kwa undani, tutavitazama kimoja kimoja katika maelezo.
MALENGO YA MTAALA.
MALENGO ni matokeo au matarajio yanayotarajiwa kupatikana kutokana na mpango/program fulani.
Mtaala wowote ule lazima uwe na malengo.
Katika Nyanja ya elimu ,malengo ya mtaala ni mabadiliko ya tabia na mwenendo wyanayotarajiwa kupatikana kwa wanafunzi baada ya kupata program fulani ya mafunzo.
UMUHIMU WA MALENGO YA MTAALA.
Malengo kama kipengele cha msingi cha mtaala yana umuhimu mkubwa kwani.
1. Huwa ni msingi wa vipengele vingine vyote viine vya maudhui ya mtaala.
2. Huwa ni msingi wa malengo katika ngazi/kiwango vyote vya elimu-elimu ya msingi, sekondari na vyuo.
3. Huwa ni msingi wa shughuri za kazi za wakuza mitaala. Wakaguzi na walimu, wanafunzi na watawala wa elimu.Malengo ya jumla ni matarajio au mabadiliko kitabia ambayo tunatarajia kuyaona kwa mtu ambae amepata elimu.Malengo ya jumla ni malengo na madhumuni ya elimu kitaifa yaliyokusudiwakutimizwa na program mbalimbaliza mafunzokatika viwango mbalimbali vya elimu. Kimsingi malengo haya yanatokana na sera ya elimu katika nchi husika.
Baadhi ya malengo ya kitaifa ni
1. kuongoza kuendeleza na kukuza vitu na uwezo wa watanzania ili waweze kutumia rasilimali zilizopo kuleta maendeleo yao binafsi na kwa Taifa zima
AY director
2. Kukuza ari ya Watanzania ili wapende kuthamini utamaduni, mila na desturi za kitanzania.
3. Kuendelezana kukuza ndani ya Watanzania moyo wa kujiamini na tabia ya kisayansi, uelewa wao na kuuheshimu.

SIFA ZA MALENGO YA JUMLA
• Huchukua muda mrefukukamilika. Mfano hadi mwisho wa program.
• Siyorahisi kuyapima kwa sababu hayako wazi.
• Huchukua vitendo kama kujua, kufahamu nk.

MALENGO MAHUSUSI
Malengo mahususi ya mtaala hutokana na malengo ya jumla. Haya ni malengo yaliyokusudiwa kutimizwa na programu mbalimbali za mafunzo katika viwango mbalimbali vya elimu.
 Ni kutokana na malengo mahususi kila kiwango cha ngazi fulani ya elimu ndiyo yanapatikana mahususi yanayowaongoza walimu katika kuandaa maazimio yao wanayofundishia darasani.
 Maudhui haya ndio yawezayo kumuongoza mwalimu kutoa maarifa na stadi ambazo zinaweza kubadili tabia ya mwanafunzi ambayo inaweza kupimika.
Kwa mfano tunapofundisha somo la Hisabati,tunatarajia kuona mabadiliko Fulani katika tabia ya mtoto kutokana na kujifunza somo zima au mada Fulani.Mabadiliko hayo yanaweza yakawa maarifa,stadi au mwelekeo mwanafunzi anaouonyesha kutokana na kujifunza somo la Hisabati ambao hakuwa nao kabla ya kujifunza somo hilo.
Tunaweza kugawa malengo mahususi katika Nyanja tatu ambazo ni
• Utambuzi
• Stadi
• Mwelekeo

SIFA ZA MALENGO MAHUSUSI
Ni malengo yaliowazi
Ni rahisi kupima kufanikiwa au kutofanikiwa kwake
Hutumia muda mfupi wa ukamilishaji wake.
Huumia vitendo kama fafanua,taja,eleza nk.

MAUDHUI
Katika kuunda maudhui ya mtaala ni vizuri kuzingatia maswali kama vile:
Ni maarifa na stadi zipi zinafaa kwa kiwango kipi cha elimu.
Ni tabia na mwenendo upi unaofaa kurithiwa.

MISINGI/ VIGEZO VYA KUCHAGUA MAUDHUI YA MTAALA
UTHABITI
Uwezo wa maudhui katika kutimiza malengo ya masomo katika kiwango husika.

UMUHIMU
Maudhui yanayopewa kipaumbele ni yale yanayolingana hali halisi ya mausha ya jamii, uchumi wan chi inayohusika. (Ni yale yenye umuhimu katika maisha ya walengwa).

MVUTO
Maudhui yafaayo ni yaleyenye kuvutia na yenye kuamsha ari ya mwanafunzi ya kupenda kufahamu maudhui hayo.
Steven George.

KUFUNDISHIKA.
Maudhui yawe na uwezo wa kufunzika/kufundishika yaani yaendane na uwezo wa walengwa.

NJIA NA MBINU.
Maudhui yazingatie mbinu na njia za kujifunzia na kufundishia

MUDA NA IDADI YA MAADA
Maudhui yazingatie muda wa program husika.Maudhui yanapoandaliwa huwakatika mfumo wamada kubwa na mada ndogo, kulingana na mfululizo huu unatakiwa uwe unaanzia na mada rahisina kuendelea hadi zile ngumu
Mpangilio wa aina hiyoni muhimu kwani huhusishaujifunzaji na ufundishaji kulingana na umri wa wanafunzi.

NJIA NA MBINU
Ili kuweza kufanikisha tando zima la ufundishaji katika kufanikisha maudhui na malengo ya somo mwalimu hutumia vitendo mbalimbali vijulikanavyo kama njia. Na njia peke yake haiwezikufanikisha somo lazima isaidiwe na mbinu.
Mbinu ni stadi maalumu inayobainisha ni jinsi gani ya kufundishia/kujifunzia itakvyowezeshwa katika tendo la kufundisha na kujifunza.
Njia ni namna mwalimu anavyowasilisha mada katika mchakato mzima wa kufundisha.
Kuna njia mbili zinazoweza kutumika katika swala zima la kujifunzia na kujifunza
Njia shirikishi
Njia isiyo shirikishi

MISINGI YA KUCHAGUA NJIA / MBINU
MAUDHUI
Hali ya somo lenyewe na maarifa ambayo mwanafunzi wanafunzi wanatakiwa wayapate hivyo maudhui yanatakiwa yafundishike.

HALI YA MWANAFUNZI
Umri wa mwanafunzi, kukomaa na kutokomaa kiakili, mazingira yao hivyo njia/mbinu ziendane na hali za walengwa.

MALENGO
Nini malengo ya wanafunzi wanatakiwa kufanikisha nini katika maisha yao? Njia/mbiu lazima zifanikishe malengo yaliokusudiwa.

MWALIMU
Uwezo mwalimu katika kutumia nji/mbinu ujuzi na utaalamu wake.

VIFAA VYA VYA MTAALA.
Mtaala una vifaa vyake maalumu ambavyo vinatakiwa vitumike kwa usahihi ili kutekeleza mtaala kwa ufanisi.
Vifaa hivyo ni:
• Muhtasari
• Vitabu vya kiada
• Vitabu vya ziada
• Kiongozi cha mwalimu
• Kitabu cha mwalimu na rejea
Muhtasari ni mwongozo unaotaja kwa kifupi tu mambo yote yanayotakiwa yafundishwe katika mwaka mzima katika darasa fukani au kwa miaka kadhaa kwa kila darasa kwa mmpangilio maalumu.
AY director

MUUNDO WA MUHTASARI
Muhtasari una sehemu kuu mbili
1. Utangulizi
2. Majedwali ya kutumia kufundishia

UTANGULIZI
Hii ni sehemu ambayohuelekeza sababu za kuwepo kwa muhtasari huo, muundo wake , malengo ya elimu katika kiwango husika na malengo ya kufundisha somo hilo katika kiwango hicho.

MAJEDWALI YA KUFUNDISHIA
Hii ni sehemu ambayo huwa na maudhui ya somo husika yanayotakiwa kufundishwa kila mwaka. Majedwali ya kufundishia yana vipengele vikuu vilivyopangwa katika safukama ifuatavyo.

VIPENGELE VYA MUHTASARI
a. Mada kuu na mada ndogo
b. Lengo la kufundishia mada hiyo
c. Mapendekezo ya njia za kufundishia na kujifunzia
d. Vifaa /zana za kujifunzia na kufundishia

MATUMIZI YA MUHTASARI
• Kumwongoza mwalimu kuandaa maazimio ya kazi na maandalio ya masomo
• Kuongoza waandishi wa kitabu cha kiada ,kiongozi cha mwalimu na vitabu vya rejea
• Kuelekeza njia zifaazo katika kufundisha na kujifunzia
• Kuandalia mwongozo wa upimaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa mwaka au kwa kipindi cha miaka kadhaa.
• Kutathmini mtaala baada ya kipindi maalumu cha matumizi ya muhtasari huo.

KITABU CHA KIADA.
Ni kitabu ambacho kinafafanua mada zote za muhtasari kwa ukamilifu. Kitabu hiki ndicho kinachobeba maudhui ya somo kwa ukamilifu.Mfano vitabu malimbali vya masomo vilivyomo mashuleni.

SIFA ZA KITABU CHA KIADA
• Kiwe chenye lugha rahisi inayo eleweka kulingana na kiwango cha mwanafunzi
• Kiwe na mada zinazopangwa kwa mtiririko wenye mantiki kuanzia mada kuanzia mada rahisi hadi zile ngumu.
• Kiwe na maandishi yanayosomeka kwa urahisi ya kuvutia
• Kiwe na maelekezo na mazoezi yanayomshirikisha mwanafunzi katika kujifunza
• Kiwe kinaendana na muhtasari pamoja na kiongozi cha mwalimu

MATUMIZI YA KITABU CHA KIADA
Mwalimu hukitumia kwa kuelekeza maarifa
Hutumiwa na mwanafunzi kwa kujikumbushia na kufanya marudio

UCHAMBUZI WA KITABU CHA KIADA
Vitabu vingi vya kiada vimeandaliwa katika mitindo tofautitofi, hivyo ni jukumu la mwalimu w somo pengine akishirikiana na wanafunzi kuchagua kitabu kinachofaa. Ili kuweza kufanya uamuzi wa kitabu kinachofaa huna budi kuchambua kwa kuzingatia mambo yafuatayo
Kwa kiasi gani mada zote za muhtasari zimefafanuliwa kwa ufanisi pamoja na kuzingatia sifa za kitabu cha kiada.
Steven George.

KIONGOZI CHA MWALIMU
Hiki ni kitabu kinachompa mwalimu maelekezo ya mada ya kufundisha jinsi ya kuifundisha , maudhui gani yafundishwe na kutumia vifaa au zana gani. Pia kinaitwa kitabu cha mwongozo kwa mwalimu.

SIFA ZA KIONGOZI CHA MWALIMU
• Kiwe na utangulizi ambao unaelekeza mambo makuu na muhimu yatakayo zingatiwa katika ufundishaji. Mfano mgawanyo wa muda katika kufundisha mada mbalimbali. Mada kuu zitakazofundishwa.
• Malengo mahsusi ya kufundisha kila mada
• Mapendekezo ya njia na mbinu za kufundishia
• Mazoezi ya kulingana na mada zilizoko katika kitabu cha kiada
• Jinsi ya kupima ujifunzaji wa wanafunzi
• Majibu ya mazoezi na na maswali yaliyomo katika kitabu cha kiada.
• Mapendekezo ya vitabu vya rejea vitakavyosaidia kutoa maarifa ya ziada kuhusu mada husika

UMUHIMU WA KIONGOZI CHA MWALIMU
• Humweleza mwalimu jambo la kufanya la kufanya humpa dira au mwelekeo wa ufundishaji.
• Humsaidia mwalimu kujijengea moyo wa kujiamini na hasa kama si mzoefu wa ufundishaji wa somo hilo.
• Humsaidia mwalimu katika kuandaa somo
• Humpa mwalimu maudhui na mifano ya ziada kuzidi kuzidi kumpanua mawazo na upeo.

DHANA YA KITABU CHA MWALIMU
Ni kitabu kinachotoa maelezo ya kina kuhusu ufundishaji wa somo fulani
Kinaelezaa jinsi ya kutenda katika hatua zote tangua uandaaji wa somo , ufundishaji hadi upimaji.
Ni mwongozo ambao unammpa mwalimu ujuzi wa ufundishaji.

SIFA ZA KITABU CHA MWALIMU
• Kina vitendo vyote ambavyo mwalimu hupaswa kutenda katika hatua za ufundishaji.
• Kinaeleza jinsi ya kutekeleza kazi ya ufundishaji hatua kwa hatua.
• Huweza kutumiwa na mwanafunzi pia
• Hutoa ufafanuzi wa mada kwa kiwango cha juu zaidi ili kupanua mawazo ya mwalimu na kumuimarisha zaidi kitaaluma.

TOFAUTI KATI YA KITABU CHA MWALIMU NA KIONGOZI CHA MWALIMU
KITABU CHA MWALIMU KIONGOZI CHA MWALIMU
01 Humwelekeza hatua za kufuata kaataika kufundisha somo au kufanya jaribio Fulani. Hupendekeza njia na mbinu mbalimbaliza kufundisha somo.
02 Huweza kutumiwa na mwanafunzi na mwalimu Hutumiwa na mwalimu tu.
03 Huhusika zaidi na mchakato au hatua za utendaji, kam vile utafitijaribio. Huhusika na jinsi ya kufundisha mada za
masomo.kwa kawaida hutumika pamoja na kitabu cha kiada.

AY director

VYANZO VYA MITAALA.
Ni muhimu kujua vyanzo vya mtaala ili kuhakikisha vinahusishwa na kuzingatiwa wakati wa kuandaa mtaala. Vyanzo hivyo ni pamoja na
1. Jamii
2. Siasa ya nchi
3. Wanafunzi
4. Wazazi
5. Walimu
6. Waajiri
7. Wataalamu mbalimbali.
Fafanua vyanzo mbalimbali vya mitaala.

Aina za Tathmini katika Ufundishaji na Ujifunzaji


Tathmini Awali – ni tathmini inayomwezesha mwalimu kuelewa mahali mwanafunzi anapostahili kuanzia katika kujifunza. Mwalimu huwauliza maswali wanafunzi na wanafunzi hujibu kwa mdomo au kwa kuandika.

Tathmini Endelevu – ni tathmini inayomsaidia mwalimu kuona kama mwanafunzi amemudu kipengele cha somo kabla kipengele kitakachofuata kufundishwa.

Tathmini Tamati – Ni tathmini inayosaidia kujua kama mwanafunzi amepata maarfa, stadi na mielekeo katika Nyanja zote za kielimu kama ilivyoorodheshwa katika muhtasari wa somo la Haiba na Michezo. Tathmini hii hufanyika mwishoni mwa kipindi cha mafunzo au baada ya mwanafunzi kumaliza ngazi Fulani ya elimu.

Tathmini Tatuzi – Ni tathmini inayomsaidia mwalimu kugundua mwanafunzi mwenye matatizo ya kujifunza yaliyoshindikana kutatuliwa na tathmini endelevu.. Mwalimu hutafuta kujua matatizo ya kujifunza aliyonayo mwanafunzi na hufanya kazi ya kumtatulia matatizo hayo mwanafunzi.

REJEA
TET (1994), Ukuzaji mitaala na
Kunasihi.KIUTA (DSM)
Wizara ya elimu na Utamaduni(2005).mpango wa mafunzo ya walimu kazini Daraja la IIIC/B-A: Moduli ya soma la Mitaala. Wizara ya elimu na Utamaduni.
TET (2013), Moduli ya kujifunzia somo la ualimu. Taasisi ya Elimu Tanzania (DSM)

Kwa mambo mengine mengi please usikose kuitembelea hihi blog yangu mstue na mshkaji aweze kupata ma notes na knowledge kibaoooo 
ASANTEEE SANA
AY director