Sunday, November 5, 2017

UPIMAJI NA TATHIMINI , Tet05207. TTC director,. AY official


UPIMAJI KATIKA ELMU

Upimaji katika elimu ni kitu muhimu sana unapotaka kujua maendeleo yaliopatikana wakati wa kujifunza au kufundisha. Upimaji humuonyesha anaejifunza ni mahali gani amefanikiwa na ni mahali gani ana mapungufu. Vilevile anaefundisha anajua ni mahali gani amefanikiwa au niwapi hajafanikiwa.
MAANA YA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Katika elimu upimaji ni tendo la kutafuta ni kwa kiasi gani mwanafunzi amepata maarifa au stadi zilizofundishwa kufuatana na malengo ya ufundishaji wa mada za somo yaliyopo kwenye muhtasari. Upimaji katika elimu pia hujumuisha mwenendo na tabia ya mwanafunzi na uwezzo wake wa kufanya mambo mbalimbali.



Matokeo katika upimaji wa elimu hutumiwa na watu mbalimbali kwa mfano mwanafunzi,shule,wazazi,waajiri walimu na watafiti.

MWANAFUNZI
Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi
Huwa ni kigezo cha chake cha kutambua ameelewa kwa kiasi gani cha kitu au vitu/ mada alizofundishwa.
Huumpa changamoto ya kujifunza. Endapo amepata alama za juu hupenda kuziendelezana kama amepata alama za chini,hufanya bidii ya kujikwamua.
Huumfanya awe makini katika kujifuza maana anajua fika kuwa atapimwa. Hii humfanya asiwe mtoro au mzembe wakati wa masomo.

MWALIMU
Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi humuwezesha mwalimu.
Kutambuwa kiwango cha uelewa wa wanafunzi katika maada mbalimbali za somo.
Kutambua matatizo wanayopata wanafunzi wakati wa kujifunza na kuyatafutia ufumbzi.
Kutambua wanafunzi wenye matatizo ya kuelewa somo au sehemu ya somo ili aweze kuwapa mafunzo ya ziada.
Kugundua malengo ya somo ambayo wanafunzi hawakufanikiwa na kuchunguza sababu.
Kuangalia mapungufu na mafanikio ya mtaala na kutoa taarifa kwa wahusika.
Kurekebisha mbinu za kujifunzia na kubuni/ kufaragua vifaa vipya ili malengo mengi zaidi yafikiwe.
SHULE
Matokeo ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi huiwezesha shule
Kujua ufanisi wake katika elimu kwa kulinganisha na shule nyingine.
Kujua malengo ya mtaala yaliofikiwa.
Kupanga wanafunzi katika mikondo (si lazima wenye uwezo mmoja wakawa pamoja)
Kumshauri mwanafunzi kuendelea na ngazi ya masomo inayofuata au kurudia.
Kushauri viongozi wa elimu kuhusu mwanafunzi anaeonekana kuwa na uwezo au kipaji maalumu ili aweze kuendelezwa.
Kuwasiliana na mzazi kuhusu maendeleo ya mwanafunzi kwa kutumia ripoti.
Kushauri wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuhusu ubora au mapungufu ya mitaala ili hatua zinazofuata zichukuliwe.
MZAZI
Matokeo ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi humwezesha mzazi
Kufahamu maendeleo ya mtoto wake
Kuchunguza chanzo cha matatizo kama yapo na kushirikiana na shule kuyatafutia ufumbuzi
Kummotisha mtoto wake ili aongeze bidii.
MWAJIRI
Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi humwezezha mwajiri;
Kuchagua mfanyakazi kwa kuangalia uwezo wake kitaaluma na mwenendo tangu akiwa shuleni.
Kumpangia mfanyakazi aina ya kazi inayoendana na uwezo wake kitaaluma.

MADHUMUNI YA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Tunaweza kuorodhesha madhumuni ya upimaji katika elimu ambayo ni;
Kujua maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma, kitabia, na kistadi.
Kubaini matatizo ya mwanafunzi katika kujifunza.
Kuangalia kiwango cha kufanikawa cha malengo ya kila mada.
Kuamsha ari ya mwanafunzi kujifunza zaidi
Kuboresha ufundishaji.
Kuandaa vigezo vya kutumia wakati wa kuchagua wanafunzi kwa masomo ya juu au kozi mbalimbali.

NYANJA ZA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Katika elimu vipengele ya kuzingatia katika upimaji ni uwezo wa kitaaluma, kufanya vitendo,na kumudu matatizo au shinikizo mbalimbali katika maaisha.
Nyanja za upimaji ni maerneo ambayo ujuzi, mwelekeo na matendo tarajiwa kwa mwanafunzi kuwa nayo,kujenga au kupata baada ya mafunzo. Nyanja za utambuzi hujumuisha
Nyanja za utambuzi
Nyanja za mwekekeo
Nyanja za vitendo

NYANJA ZA UTAMBUZI
Nyanja hiii inahusika na ujuzi /uzoefu ambao mwanafunzi anatarajiwa kuwa nao baada ya kujifunza na kupewa mtihani au majaribio. Nyanja hii Benjamin Bloom (1956) ameigawa katikavifungu (ngazi) sita vilivyopangwa kuanzia kifungu kilicho rahisi hadi kilicho tata. Vifungu hivyo ni
Maarifa
Ufahamu
Matumizi
Uchambuzi
Uunganishaji/ uundaji
Tathimini

NGAZI YA MAARIFA
Maswali yanayoulizwa hupima uwezo wa mwanafunzi kukumbuka maarifa, stadi za jumla alilzojifunza.(Je, mwanafunzi anaweza kukumbuka alichofundishwa?). Vitenzi vinavyotumika katika maswali yanayopima ngazi hii ni kama , Taja, andika, orodhesha, eleza.
Mfano wa maswali ni kama
Taja makundi mawili ya viumbe hai
Orodhesha mambo yanayoathiri kinga ya mwli
Nini maana ya mashine?

NGAZI YA UFAHAMU
Mwanafunzi anapimwa katika ngazi hii ni kutaka kujua kama anaweza kuhusisha maarifa mapya na marifa aliokuwa nayo.(Je,mwanafunzi anaweza kukueleza nakutafsiri maana ya kitu kilichofundishwa?) Vitenzi vinavyotumika katika maswali yanayopima ngazi hii ni kama Toa, fupisha, eleza.
Mfano wa maswali ni kama
Toa tofauti kati ya wanyama na mimea.
Eleza athari za UKIMWI katika jamii.

NGAZI YA MATUMIZI
Ngazi hii huhusisha maswali yanayomtaka mwanafunzi kutumia habari anayoifahamu kupata jibu. (Je, mwanafunzi anaweza kutumia maarifa na stadi katika mazingira mapya kuhusu mambo aliyofundishwa?) Vitenzi vinavyotumika katika maswali yanayopima ngazi hii ni kama
Kokotoa mlinganyo ufuatao
2x+y= 1 na 2x-y=2
Elezea kwa ni meli inaelea juu ya maji.

NGAZI YA UCHAMBUZI
Ngazi hii mwanafunzi hutakiwa kufikiri kwa makini na maswali yanayotungwa ni yanayomtakaka mwanafunzi kuchambua maarifa na kubainisha sehemu zake na kuonyesha uhusiano.(Je, mwanafunzi anaweza kutambua na kuhusianisha sehemu mbalimbali za kitu au taarifa?).
Mfano wa vitenzi vinavyotumika ni kama kuhusianisha,changanua, gawanya,tenga.
Mfano wa maswali ni kama
Kwa nini karafuu haiwezi kustawi Lushoto?
Andika kwa kifupi kifungu cha habari kifuatacho.
Chora ramani ya Tanzania na uoneshe maziwa ma mito.

NGAZI YA UUNDAJI
Katika ngazi hii mwanafunzi hupimwa uwezo wake wa kuunganisha vitu mbalilmbali kuunda kitu kizima.(Je mwanafunzi anaweza kutoa uamuzi au kuanzisha mambo kutokana na taarifa zilizochanganuliwa?) Vitenzi vinavyotumika ni kama husianisha, jenga upya, pangilia, unda fupisha. Mfano wa maswali ni kama
Hatua gani zichukuliwe ili kupunguza matatizo kwenye utafiti?
Eleza namna utakavyoboresha mazingira yaliyoharibika kwa ajili ya ukataji miti.

NGAZI YA TATHMINI
Katika ngazi hii mwanafunzi anatakiwa kutathmini uzuri au ubaya wa matumizi ya kitu fulani na kufanya maamuzi.(Je,mwanafunzi anaweza kuamua kitu kina thamani gani au kinafaa au hakifai kufuatana na kipimo sanifu kuchunguza sifa za kitu hicho). Vitenzi vinavyotumika ni kama hakiki, hitimisha, kubaliana, tetea, toa ufupisho, toa makosa.
Mfano wa naswali ni kama
Elimu ni bora kuliko mali. Je, unakukbaliana na usemi huu? Eleza jibu lako.
Fafanua kauli hii kwa kutumia hoja tano. Utafiti wa matumizi ni bora zaidi kuliko utafiti wa msingi.
Steven Georges’ property

NYANJA YA MWELEKEO
Ni nyanja ya malezi ya hisia ambayo inahusika katika kupima tabia ya mwelekeo na mwenendo wa mwanafunzi. Lengo ni katika kujua; usafi, ushirikiano, uvumilivu juhudi na kujadili mambo.
NGAZI ZA NYANJA YA MWELEKEO
Ngazi ya kuwa tayari kupokea mambo mbalimbaali
Ngazi ya kushiriki/ kuitikia
Ngazi ya kutathmini na kuhusianisha
Ngazi ya msimamo/ Ngazi ya kuoanisha maswala mbalimbali
NGAZI YA KUWA TAYARI
Hii ni ngazi ya kwanza ambayo huonesha utayari alionao mwanafunzi kujifunza.(Je, mwanafunzi yuko tayari kupokea kichokoo,kwa mfano kukubali kushauriwa?). Vitenzi vinavyotumika ni kama chagua jibu sahihi, elekeza, fuata.
Mfano wa maswali ni kama
Utakapochelewa kipindi cha ualimu utafanya nini?
Uko tayari kusoma na mwanafunzi mlemavu
NGAZI YA KUITIKIA / KUSHIRIKI
Katika ngazi hii mwanafunzi yuko tayari kujifunza, kuonyesha mwitikio alionao kama kwa kuwa mchangamfu muda wote.(Je, mwanafunzi anaweza kushiriki katika shughuri mbalimbali yaani kuchangia mawazo na utendaji?) Vitenzi vinavyotumika ni kama amkia, saidia tambulisha, simulia, nyumbulisha . Mfano wa maswalli ni kama
Utamsaidiaje mtu alieumwa na nyoka?
Ngoma zinapochezwa usiku zinachochea maambukizi ya UKIMWI. Jadili
NGAZI YA KUTHAMINISHA
Mwanafunzi hupimwa jinsi gani anavyojisamini yeye mwenyewe, anavyothaminiwa na wenzake walimu wake na jami ikwa jumla.(Je mwanafunzianaweza kuthamini kitu wazo na watu yaani kuwajibika?) Vitenzi vinavyotumika ni kama fanya kazi, toa taarifa, shirikiana, pendekeza, pambanua.
Mfano wa maswli ni kama.
Badili asilimia kuwa desimali
Oanisha maneno kwenye orodha A nay ale yalioko kwenye orodha B.
KUOANISHA MASWALA MBALIMBALI
Mwalimu hupima uwezo wa mwanafunzi katika kulinganisha na kutofautisha vitu mbalimbali.(Je,mwanafunzi anaweza kuwa na msimamo wa fikra?) Vitenzi vitumikavyo ni kama; Unda, zingatia, husianisha tayarisha unganisha, linganisha.
Mfano wa maswali ni kama
Binadamu wote ni sawa thibitisha kauli hii.
KUWA NA MSIMAMO
Mwalimu kupima msimamo wa wanafunzi juu ya maamuzi ya maswala mbalimbali
NYANJA YA STADI
Kipengele hiki hupimwa kwenye vitu vinavyohusu utumiaji wa mikono,miguu, na sehemu nyingine za mwli. Vitu muhimu vinavyoangaliwa ni kama uwezo wa
Kutumia vifaa au zana
Kuchagua vifaa au zana muafaka
Kutunza au kurudisha vifaa/zana mahali pake
Kupata matokeo mazuri au zao bora
Nyanja ya stadi imegawanyika katika ngazi kuu tatu ambazo ni
Kuchunguza
Kuiga
Kurekebisha
KUCHUNGUZA
Je, mwanafunzi anaweza kuangalia na kusikiliza kwa makini kinachotendeka?
KUIGA
Je, mwanafunzi anaweza kkufuatisha maelekezo kwa vitendo ili kujenga mazoezi ya utendaji?
KUREKEBISHA
Je mwanafunzi anaweza kutumia misingi ya utendaji kubuni kitu kipyaau utendaji mpya?
Steven Georges’ property
ZANA ZA UPIMAJI KATIKA ELIMU
Zana kuu zinazotumika katika upimaji wa maendeleo ya elimu ni pamoja na mazoezi, mitihani, muongozo wa usaili,majaribio na jedwali la kupima tabia na mwenendo wa wanafunzi.
MAZOEZI
Unapokuwa unafundisha kwa njia shirikishi ni jambo la kawaida kuwauliza wanafunzi wako maswali. Maswali haya huwa ni sehemu ya mazoezi ya kujenga somo. Vilevile hukupa mwanga ni mwanafunzi gani anafuatana na wewe unavyofundisha. Si kila mwanafunzi atapata nafasi ya kujibu maswali, njia hii haitoshi kupima ufundishaji.Ili kufanya ikamilike inabidi utoe zoezi kila amalizapo dhana,mada au sura.
MAJARIBIO
Majaribio ni mazoezi yanayotolewa na mwalimu kwa mwanafunzi ili kumpima mafanikio yao katika kujifunza. Majaribio hufanyika kuwapima wanafunzi katika mada kuu au mada nyingi.Majaribio haya hufanywa mara moja kwa kila majuma mawili, mwezi au nusu mhula, Njia hii huweza kumpima mwanafunzi anavyoendelea kupokea na kuhifadhi taaluma.
MITIHANI
Mitihani hutolea kwa shule za msingi, sekondali, vyuoni mwishoni mwa mhula. Matokeo ya mitihani huonyesha mwanafunzi anavyoendelea katika masomo yake mbalimbali iklinganishwa na wenzake.
Mitihani mikuu inayofanyika ni pamoja na
Mtihani wa kualilza darasa la saba ambao hutumika kuchagua wanafunzi kuingia sekondari kikdato cha kwanza.
Mtihani wa kidato cha pili.
Mtihani wa kkumaliza kidato cha nne ambao hutumika kuchagua wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na watakao fanya kozi mballimbali za kitaaalam
Mtihani wa kidato cha sita ambao hutumika kuchagua wanafunzi watakaoendelea na masomo zaidi ya sekondari ikwapo vyuo kikuu.
JEDWALI LA TABIA NA MWENENDO
Ni jukkumu la mwalimu kumlea mwanafunzi awapo shuleni. Hivyo inakubidi ujue tabia na mwenendo wake kila mara. Ili kuweza kufanya hivyo inakubidi kuwa na jedwali la kuchunguza mwenendo na tabia wa wanafunzi.
Steven Georges’ property
JEDWALI LA KUPIMA TABIA NA MWENENDO WA WANAFUNZI
GREDI
MAELEZO
Darasani
Huwahi kuingia darasani
Hufanya kikamilifu kazi anazopewa
Hushirikiana na wenzake katika masomo
Huondoka tu baada ya kumaliza kazi
Tabia nyingine.
Hutmiza majukumu anapopewa nafasi ya kuongoza wenzake
Ana heshima kwa walimu, watu wengine na wanafunzi wenzake
Anatunza usafi wa mwili wake na mavazi
Ni mwaminifu
Anafanya kazi kwa bidiii na stadi
Huonwa na wanafunzi wenzake kwa ushauri
Shughuri za ujenzi wa taifa
Hushiriki bila kinyongo katika kazi za ujenzi wa taifa, shuleni na nje ya shule
Hushirikiana na wenzake katika kukamilisha kazi iliyotolewa
Huwatia moyo wenzake katika kukamilisha kazi iliyotolewa
Mambo mengineyo
Anashiriki kikamilifu katika kukamilisha kazi aliyopewa
Anashiriki kikamilifu katika shughuri za utamaduni
Tumia A,B,C,D,E kupima mwanafunzi katika safu ya gredi
Ufunguo; A= Vizuri sana, B=Vizuri, C= Wastani, D= Dhaifu, E=Mbaya.
Wakati unapojaza jedwali unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo
Usiwe na jazba kutokana na tukio moja.Chunguza kwa muda endapo tukio limekkuudhi
Mshirikishe mwalimu mwenzako endapo anamjua zaidi mwanafunzi
Usitoe upendeleo
Steven Georges’Property
MWONGOZO WA USAILI
Upimaji kwa kusaili hufanyika ana kwa ana. Unapopata mwanafunzi mgeni na unapenda kujua uwezo wake au historia ya alikotoka unaweza kumuita na kuongea nae. Ili uhakikishe mambo yote unayoyataka kujua unayauliza ni vizuri kuandaa mwongozo wa usaili.
Mwongozo wa usaili haya ni maswali yalioorodheshwa kwa mpangilio maalum ili kuwa na mtiririko mzuri wa mawazo. Usaili huu pia huweza kutumika kuchunguza matatizo ya mwanafunzi katika kujifunza.
Steven Georges property
UTUNZI WA MAJARIBIO NA MITIHANI
Misingi ya utunzi wa majaribio na mitihani
majaribio na mitihani yana umuhimu mkubwa sana katika upimaji wa maendeleo ya wanafunzi. Yanajumuisha vitu halisi vinavyotarajiwa na mwalimu kutoka kwa wanafunzi baada ya kujifunza/ ujifunzaji.
Dhumuni kubwa la majaribio na mitihani ni
1.Hutupatia taarifa kamili na halisi kuhusu maendeleo ya mwanafunzi. Mwalimu anatakiwa kutoa majaribio na mitihani kwa wanafunzi ili kujua kile kinachotakiwa kupimwa kwa wakati ule. Mwalimu anpoazimia kutunga jaribio/ mitihani anatakiwa kufuata hatua zifuatazo.
Mwalimu anapaswa kufahamu vema mambo anayotaka kuyapima. Kitendo hicho kitakufanya ufanye uamuzi kuhusu maswali utakayo yatumia.
Maswali ya mitihani yagusie vipengele vingi vya maudhui yaliofundishwa kwa kipindi hicho.
Mwalimu aamue ni aina gani ya maswali atakayoyatumia. Kimsingi kuna aina kuu mbili za maswali, maswali ya kujieleza ambayo yanadai majibu yatolewe na mtahiniwa lakini kiwango cha usahihi wa majibu hayo yanatolewa na mtahini. Maswali haya yanataka mtahiniwa kujua kweli ya mambo mbalimbali na kuonyesha mambo yanayohusiana na yasio husiana. Utoaji wa majibu katika maswali ni kwa kutumia insha au majibu mafupi. Aina ya pili ya maswali ni maswali yakinifu. Maswali haya yanamtaka mtahiniwa kutambua jibu lililosahihi miongoni mwa majibu yaliotolewa na mtahini. Katika maswali haya mtahiniwa hana uhuru wa kuchagua majibu mengine yalio tofauti na yale yaliotolewa.
JEDWALI LA KUTAHINI
Kabla mwalimu hajaanza kutunga maswali anapaswa kutayarisha jedwali la kutahini. Jedwali la kutahini ni utaratibu unaonyesha maada za kupima na idadi ya maswali kwa kila maada. Jedwali hili huonyesha malengo yanatarajiwa kufikiwa pamoja na idadi ya maswali kwa kila maada. Jedwali hupangwa kwa safu. Safu ya kwanza upande wa kushoto huwekwa maudhui kwa kuorodhesha maada zinazopimwa. Safu inayofuata kulia huwekwa malengo ya kupimwa.
Watahini wengi hutumia mgawanyo wa bloom (1956) kuainisha stadi hizo. Hata hivyo hufungwi na utaratibu huu ikiwa somo lako haliwezi kupimwa kikamilifu kwa mgawanyo huo.unaweza kuweka utaritibu mwingine kama utaona unafaa zaidi.
Idadi ya maswali huonyeshwa katika mkato wa chumba cha maudhui kuelekea kulia na kile cha safu ya stadi zinazopimwa.
Jumla ya maswali kwa kila maada huandikwa upande wa kulia. Jummla ya maswali kwa kila ngazi ya utambuzi huandikwa kwenye mstari wa chini ya jedwali.
STADI ZA KUPIMWA
1
2
3
4
Jumla
Asilimia kwa kila
Maada za kupimwa
Maada za kupimwa
Jumlaya maswali
Asilimia kwa kila ngazi
UTAYARISHAJI WA JEDWALI LA KUTAHINI
Mambo ya kufanya wakati wakuandaa jedwali la kutahini
1.Chukua muhtasari wa somo na maandalio ya somo
2.Chunguza katika maandalio ya somo maada ambazo zimekishwa fundishwa
3.Chagua mada ambazo unaona ni muhimu zitungiwe jaribio/ mitihani kisha orodhesha mada hizo.
4.Chunguza kwa makini katika muhtasari na maandalio ya somo ya somo malengo mahsusi ya mada zinazotungiwa maswali
orodhesha malengo hayo kisha amua
i/ aina ya maswali yatakayotumika katika upimaji
ii/ idadi ya maswali yote katika mtihani
iii/ muda wa kufanya jaribio hutegemea na wingi wa mada na hali ya malengo yenyewe 5. chora jedwali la kutahini
6.jaza jedwali la kutahini kwa kufuata hatua hizi
i/ orodhesha mada zote za kutungiwa maswali.
ii/ orodhesha malengo mahususi katika safu inayofuata
iii/ Amua ngazi zipi za nyanja ipi za kupimwa zipewe umuhimu wa kupewa maswali mengi na zipi zipewe maswali machache.
UMUHIMU WA JEDWALI A KUTAHINI
I/ Linahakikisha kuwa maudhui yote yanayotakiwa kutahiniwa yanatahiniwa.
Ii/ Linahakikisha kuwa kiwango cha kuelewa maarifa , kumudu stadi za utendaji na kubadilika kwa mwelekeo wa watahiniwa kinatahiniwa
iii/ Linahahakikisha uwiano wa idadi ya maswali katika kila eneo na kila kipengele cha nyanja kinapimwa .
Mfanowa jedwali la utahini kwa somo la maarifa ya jamii darasa la tano katika nyanja ya mwelekeo
STADI ZA KUPIMWA
MADA Z KUPIMWA
MALENGO YA KUPIMWA
Kuwa tayari
kuitikia
Kutathmini
Kuwianisha maswala
Msimamo
Jumla
% kwa kila mada
Mahusiano ya jamii za Tanzania
1
2
3
15%
Mila na desturi
1
1
1
3
15%
Kufanya kazi
1
1
1
3
15%
Kusoma ramani
1
2
3
15%
Muundo wa serikali ya kijiji
2
1
3
15%
Ushiriki wa jamii
2
3
5
15%
Idadi ya maswali
5
6
2
4
3
20
15%
% kwa kila ngazi
25%
30%
10%
20%
15%
100%
100%
UCHAMBUZI WA TAFSIRI YA MATOKEO YA MAJARIBIO NA MITIHANI
Baada ya mwalmu kusahihisha jaribio / mtihani na kutoa alama hatua inayofuata ni uchambuzi wa tafsiri ya jaribio/ mtihani.
Kuna mambo mawili makubwa yanayojumuishwa ;
i.Kufanya uchanganuzi na tafsiri ya takwimu ya maksi (alama) inayokusudiwa kutathimini kiasi cha mafanikio ya utendaji wa mtahiniwa.
ii.Kufanya uchanganuzi wa maswali ya jaribio ili kuona iwapo jaribio lilitumika kupima ufanisi wa utendaji wa watahiniwa katika nyanja mbalimbali za kujifunza lilifaa kwa kiasi gani.
UCHAMBUZI WA MATOKEO YA MTIHANI NA TAFSIRI
Uchambuzi wa matokeo ni mchakato mzima wa kurekodi kuzipanga alama kulingana na mahitaji ya mtumiaji .
MADHUMUNI YA KUCHAMBUA
Kuelewa ujuzi uliotarajiwa kujengwa na mwanafunzi kama ilivyokusudiwa.
Kupima mafanikio ya kazi ya mwalimu.
UMUHIMU WA KUCHAMBUA NA KUTAFSIRI DATA
Inamsaidia mwalimu kujitathimini mwenyewe katita utendaji wa kazi
Inamsaidia mwalimu kufahamu viwango vya ujuzi walionao wanafunzi
Inamsaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya mbinu na njia za kufundishia
Inamsaidia kupanga mikakati ya kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kujifunza
Inasaidia wanafunzi kujitathimini wao wenyewe kwa kufahamu maeneo wanayoyamudu na wasiyoyamudu.
Inatoa nafasi kwa jamii kuelewa/kufahamu jinsi ya kufanya marekebisho juu ya mitaala.
Istilahi zinazotumika katika kuchambua matokeo ya mitihani ni ukokotoaji wa :Wastani, modi, mfiko alama yakati (mediani ).
Wastani
Wastani ni kiwango cha kati cha hesabu.
Hupatikana kwa kujumlisha maksi zote halafu kugawanya kwa idadi ya watahiniwa.
i.e
Wastani = Jumla ya alama
Idadi ya watahiniwa
Endapo alama zimetolewa kwa jedwali la marudio, idadi ya watahiniwa ni
X=∑fx/∑f
Mfano 12,24, 36, 25.
Alama
Chale
Marudio
fx
67
1
1
67
66
1
1
66
64
1
1
64
61
1
1
61
55
11
2
110
45
1
1
45
35
1
1
35
27
1
1
27
25
1
1
25
Dosari za alama za wastani
Haituelezi ubora au ufanisi wa kujifunza na maendeleo ya wanafunzi.
Manufaa ya alama ya wastani
Hutumika kutafuta ukatikati wa maendeleo ya mwanafunzi.
Hutusaidia kutupa picha ya maendeleo ya mwanafunzi ikiwa idadi ni kubwa.
MODI
Modi ni alama iliyojitokeza mara nyingi kupita alama nyingine. Ni alama yenye marudio (f) mengi zaidi.
Mfano 23,33,24,24,32,25,22,24,26 na 25.
modi yaweza kuwa ni namba moja au zaidi ya moja endapo marudio yanalingana au hakukua na alama zisizojirudia.
MFIKO
Mfiko ni tofauti iliyopo kati ya alama ya juu kabisa na alama ya chini kabisa katika seti ya maksi za watahiniwa. Mfano
tafuta mfiko kwa alama zifuatazo
73,35, 42, 85, 36 na 78
Mfiko = 85-35=50
Endapo mfiko (range) ni ndogo, tafsiri yake ni kuwa watahiniwa walikuwa nauwezo uliokaribiana au unaokaribia kulingana.
Endapo mfiko ni mkubwa hiyo inaonyesha kuwa watahiniwa wana uwezo tofauti, yaani wapo wenye uwezo wa juu zaidi na wapo wenye uwezo wa chini zaidi.
UWEZO WA SWALI KUPAMBANUA
Katika upimaji, swali zuri ni lile ambalo wanafunzi walio hodari wenye uelewa na ujuzi wa kiwango cha juu zaidi kitaaluma watalifanya vizuri na wale wenye kiwango cha chini zaidi kitaaluma wtalifanya vibaya.
Hii ina maana kuwa swali zuri(pamoja na sifa au vigezo vingine) ni lazima liwe na uwezo wa kupambanua wanafunzi walio hodari na wasio hodari.
Namna ya kukokotoa uwezo wa swali kupambanua
1. Panga wanafunzi kuanzia alama za juu hadi za chini
2.Gawa watahiniwa katika makudi matatu. H: maksi za juu (1⁄3N), kundi la kati (1⁄3N) na L. maksi za chini (1⁄3N).
sampuli ya uchanganuzi ambayo hasa ndio inayohusika na ukokotozi wa upambanuzi wenyewe huitwa T, nayoundwa na kundi la Juu la H na lile la chini L.
T= H+L
3.Kokotoa uwezo wa kupambanua (D) kwa kutumia kanuni hii
D =RH-RL⁄½T
Wakati D= ni uwezo wa swali kupambanua
RH= ni idadi ya H waliopatwa swali.
RL= ni idadi ya L waliopatwa swali
T= ni idadi ya walioshirikishwa. Kundi shiriki ambalo ni (1⁄3N) ya juu na (1⁄3N) wa chini
mfano wa ukokotozi.
Kwenye mtihani uliofanywa na wanfunzi 18, wanafunzi 4 bora walipata swali la tano na wanfunzi 2 duni walipata swali hilo.
Kutoka kwenye kanuni
D =RH-RL⁄½T
H= 1/3* 18= 6
L= 1/3* 18= 6
T= H+L=12
D= (4-2/½*12)= 2/6
D= 0.3
Kwa hiyo kiwango cha ugumu wa swali mla 5 D5= 0.3.
unapopata D= +1; hii ni namba ya juu kabisa. Namba hii tafsiri yake ni kuwa wanafunzi wote hodari wamelipata swali na wasio hodari wamelikosa.
Ukipata D= 0 hii ina maana kuwa swali husika halina uwezo wowote wa kupambanua.
Endpo D=-1 tafsiri yake ni kuwa wa wanafunzi wengi wenye uwezo wa chini wamelipata swali hilo ukilinganisha na wanafunzi wenye uwezo wa chini. Swali au maswali kama hayo hayafai kwenye mtihani.
Mwongozo wakutambua maswali ya mtihani yalio bora
Kiwango cha D
Tafsiri yake
Uamuzi wa kuchukua
0.4 na zaidi
Swali linafaa
Libaki katika mtihani
0.2- 0.39
Haliridhishi
Lilekebishwe kisha lijaribiwe tena,
0.1- 0.19
Halilidhishi
Liondelewe katika mtihani
D=-(Hasi)
Halilidjishi
Liondelewe katika mtihani

Kwa Mabo mengine mazuri na matamu zaidi usikose kuitembelea blog yangu
AY director

No comments:

Post a Comment